Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KIWANDA CHA URAFIKI CHAPEWA MDA WA KUWAONGEZEA MISHAHARA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Serikali imeupa uongozi wa Kiwanda cha Urafiki hadi Desemba mosi, mwaka huu kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi ya kuanza kuwalipa nyongeza ya mishahara wafanyakazi wake kama sehemu ya kumaliza mgogoro wa wafanyakazi uliodumu kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Wiki iliyopita, wafanyakazi wa kiwanda hicho walifanya mgomo endelevu wakidai nyongeza ya mshahara.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, alipotembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi na wafanyakazi.

Alisema kila mfanyakazi katika kiwanda hicho ana haki na mamlaka ya kudai anachostahili bila kupingwa na mtu yeyote na vile vile ana haki ya kusikilizwa na kutimiziwa mahitaji yake yote muhimu na kwa muda unaostahiki.

Licha ya kutoa agizo hilo, pia DC Makonda aliutaka uongozi wa kiwanda hicho na Chama cha Wafanyakazi kukaa kwa pamoja ili kubaini deni sahihi la wafanyakazi kwani kiwango cha deni la sasa kinaonekana kuwa na utata.

Kabla ya kuwalipa madai wafanyakazi hawa, nahitaji pande zote mbili zikae pamoja kwa majadiliano ili kupitia madai upya hatimaye kujua wafanyakazi wanadai kiasi gani,? alisema.

Aidha, Makonda ameagiza kila mfanyakazi husika kupata malipo yake uwe wazi.
Wakizungumza na Nipashe kiwandani hapo muda mfupi baada ya serikali kutoa maelekezo hayo, baadhi ya wafanyakazi hao walisema wamepata matumaini ya mgogoro kufikia mwisho na kumpongeza Mkuu wa Wilaya kwa jitihada alizofanya.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top