Featured

    Featured Posts

Loading...

WATU WATANO WAUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Watu watano wamefariki dunia papo hapo kwa kukatwa katwa mapanga na kuchinjwa kama wanyama katika kitongoji cha Kisesa kata ya Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

Watu hao ambao ni wa familia moja walifanyiwa unyama huo kwa kukatwa katwa mapanga sehemu ya shingoni.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Gemine Mushy alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9 ambapo Baba, Mama pamoja na watoto wao 3 waliuawa.

Mushy aliwataja waliofanyiwa unyama huo kuwa George Charles (30) ambaye ni Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote wasukuma wa kitongoji hicho.

Kamanda Mushy alieleza chanzo kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu (George) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi alikokuwa akiishi marehemu.


Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya msako na kuwakamata watuhumiwa 3 ambao aliwataja kuwa ni Migata Lusalago (50) Jihelya Migata (30), Solo Kengele (31) wote wasukuma wa kijiji cha Bugalama.

Kamanda mushy alieleza kuwa waliokamatwa ni Baba wa kambo wa Marehemu pamoja na watoto wake wawili ambao ilidaiwa kuwa wameweza kushiriki katika kutenda tukio hilo la kinyama.

Katika hatua nyingine Mushy alisema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika ili kuwapata wahusika zaidi wa tukio hilo.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top