Abiria waliokuwa wakisafiri kwa gari moshi kupitia reli ya kati
wamekwama kwa saa kumi na sita katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam huku wakilalamikia kutelekezwa na shirika la reli
Tanzania katika sehemu ambayo hakuna huduma muhimu za kijamii.
Baada ya ITV kupata fununu kuhusu kukwama kwa gari moshi hilo lenye
jumla ya mabehewa 12 kuelekea mikoa mbalimbali, tulifika katika eneo la
pugu na kukuta baadhi ya abiria wakiwa wamechoka kutoka na njaa huku
wengine wakiwa wamelala, na wengine wakipaza sauti zao kulalamikia
kitendo cha kutelekezwa katika eneo hilo huku viongozi wahusika wa treni
hiyo wakikimbia.
Baadhi ya wagonjwa nao wakatupa lawama kwa shirika la reli Tanzania
kwa kuwatelekeza huku wakihofia maisha yao na maisha ya watoto katika
eneo hilo.
Meneja uhusiano wa shirika la reli Tanzania ambaye licha ya kukiri
kuwepo kwa ajali ya Treni ya mizigo kati ya Soga na Pugu, alishindwa
kueleza vizuri sababu zilizowafanya viongozi walikuwa wakisafiri na
treni hiyo akiwemo mkuu wa kituo cha Pugu kukimbia na kufunga ofisi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies