9.30am:Chama cha CCM kinachoongozwa na mgombea wa
urais John Magufuli kimeshinda majimbo yote ya ubunge katika eneo la
Dodoma huku Muungano wa Ukawa chini ya uongozi wa Edward Lowassa
ukichukua viti vingi katika mji wa Dar es Salaam.
9.00am:NEC yatoa ufafanuzi kuhusu matokeo
Mwenyekiti
wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya
ucheleweshaji wa matokeo ya rais kutoka majimbo mbalimbali akisema
kuwa tume hiyo inatoa matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi
katika majimbo yote nchini..
7.00am:Washerehekea Kinondoni
Kulikuwa na sherehe katika jimbo la Kinondoni nchini Tanzania baada ya chama cha CUF kushinda katika eneo hilo.
Vijana waliokuwa wakifurahia ushindi huo waliimba na kuzunguka na bajaji wakiusifu ushindi huo na chama chao.
Hatahivyo maafisa wa polisi katika eneo hilo walifika katika eneo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea.
6.00am:Hali ya wasiwasi yatanda Zanzibar
Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.
Vyombo
vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya
sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza
kuwa mshindi.
Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha
CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi
yake.
UMEAMKAJE?
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini
Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu
matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza
matokeo ya majimbo takriban 100 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.
Tunafuatilia pia hali ilivyo Zanzibar baada ya
mtafaruku jana kuhusu kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wakati mmoja
maafisa wa usalama walizingira kituo kinachotumiwa na Tume ya Uchaguzi
Zanzibar kutangaza matokeo na hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka.
Tume ya uchaguzi humo visiwani kufikia jana jioni ilikuwa imetoa matokeo
ya
majimbo 31 kati ya majimbo yote 54.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies