Jeshi la Polisi limekita kambi Temeke mikoroshini kata ya Sandali jimbo
la Temeke baada ya hali kuelezwa kuonekana tofauti kutokana na vijana wa
eneo hilo kujaa kwa wingi kwa kile kinachoelezwa wanataka matokeo
yatangazwe kwani wana wasi wasi na utangazwaji wa matokeo.
Wananchi hao wanadai kuwa wana wasiwasi kutangazwa matokeo tofauti wakati wanaamini mgombea wao kutoka CUF atakuwa kashinda dhidi ya CCM,lakini bado mawakala hawajaweka wazi matokeo hivyo hadi sasa.
Kwa Mujibu wa
muandishi wetu Sam Mahela aliyepo eneo hilo anayefuatilia taarifa hizi
za uchaguzi anasema kuwa licha ya jeshi la polisi kuwepo eneo hilo
linahakikisha hakuna tatizo lolote linalo tokea na kuona wasimamizi
wakitangaza matokeo bila hofu. Source ITV
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies