Jenerali Gilbert Diendere ,kiongozi wa mapinduzi ya mwezi uliopita nchini Burkina Faso anazuiliwa na vikosi vya usalama vya taifa hilo.
Baadhi ya ripoti zinadai kuwa awali alikuwa amesalimu amri katika ubalozi fulani ndani ya mji mkuu wa Ouagadougou.
Kaimu wa rais Michel Kafando alirudishwa mamlakani wiki iliopita kufuatia kuingilia kati kwa jeshi pamoja na viongozi wa Afrika Magharibi.
Kikosi cha walinzi wa rais kilichotekeleza mapinduzi hayo kinatarajiwa kuvunjwa.
Jenerali Diendere amewasilishwa kwa mamlaka ya Burkinabe,kulingana na duru za mahakama.
Awali kiongozi huyo alikuwa amekimbilia hifadhi katika afisi ya mwakilishi wa Vatican nchini humo.
Hatahivyo maelezo zaidi ya kusalimu amri bado hayajulikani.