Featured

    Featured Posts

Loading...

MWENYEKITI WA CUF NA WENGINE 16 MBARONI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Bukoba. Jeshi la Polisi limewakamata watu 16 akiwamo Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Bukoba kwa madai ya kuhusika na vitendo vya uchomaji wa makanisa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bukoba.

Watu hao, wakiwamo viongozi na wanachama wa CUF, walikamatwa juzi na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Kagera na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Augustine Ollomi aliwaeleza waandishi wa habari kuwa atalitolea ufafanuzi suala hilo leo.

Waliokamatwa katika tukio hilo, ni diwani aliyemaliza muda wake Kata ya Katoro (CUF), Amini Mashaka, Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Bukoba Vijijini, Ladslaus Kashonda, Rwegasira Kashonda, Abdul Dauda, Mwalimu Shakuru Katakweba, Sulaiti Katima, Mudathiru Rukindo, Hashimu Kanyonyi, Abdul Nkingireha, Sadiq Mustafa, Hassan Bakuza, Suleiman Mfuruki na mwingine aliyetambulika kwa jina la Jasson.

Mgombea ubunge wa CUF, Jimbo la Bukoba Vijijini, Buberwa Kaiza alidai kuwa wote waliokamatwa ni viongozi wa chama hicho na wamebambikizwa tuhuma za kuchoma makanisa na kukamatwa usiku wa kuamukia leo.

Kaiza alisema kwa mtu anayejua mwelekeo wa kampeni za ubunge na udiwani katika kata za Katoro, Nyakibimbili, Kasharu, Kaibanja na Kishogo atakuwa anafahamu kuwa masuala hayo yanahusiana na masuala ya kampeni.

Hofu ya wananchi
Wakazi wa Kata za Katoro na Kaibanja ambako yalitokea matukio matatu ya uchomaji wa makanisa usiku wa kuamkia Jumapili, walisema suala hilo limeleta hofu zaidi kwa kuwa hata kundi lililokuwa linacharaza wananchi na kuharibu mali kabla ya hapo halikuwahi kujulikana, huku wengine wakisema ni la kisiasa.

Pamoja na matukio ya uchomaji kutokea katika Kata ya Kaibanja, watuhumiwa zaidi ya 15 waliokamatwa wakihusishwa na matukio hayo wote wanatoka kata jirani ya Katoro.

Baadhi ya wananchi wameshangaa kukamatwa kwa mgombea udiwani wa Katoro, Mashaka akihusishwa na uchomaji wa makanisa wakati amewaongoza kwa vipindi viwili mfululizo sasa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaibanja, Muganyizi Bagandanshwa alihusisha vitendo vya uchomaji wa makanisa na kuibuka upya kwa kundi la ‘wakacharaji’.

Bagandanshwa alisema vitu vilivyoteketezwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Mtaa wa Kaibanja vina thamani ya zaidi ya Sh2 milioni na vilikusanywa eneo anaposimama kiongozi wa ibada kabla ya kuteketezwa.

Mchungaji wa Kanisa la Faith Mission lililopo katika Kijiji cha Kaibanja, Laurent Komba alisema yeye na waumini wake wanaishi kwa hofu wakiamini matukio yaliyotokea kwenye makanisa jirani yanaweza kuwafikia pia.

USULI
Katika matukio matatu tofauti ya kuamkia Jumapili, makanisa matatu yalichomwa moto. Mbali na lile la Kilutheri, mengine ni Kanisa Katoliki lililopo katika Kijiji cha Kijongo na Pentekoste Buhaya la Kijiji cha Musira.

Wiki iliyopita polisi waliwatia mbaroni watu saba kwa tuhuma za kuhusika na uchomaji moto wa makanisa matatu mjini Bukoba.

Makanisa hayo ni Pentecoste Assemblies of God (PAG) lililopo Mtaa wa Buyekera, Living Water na Evangelical Assemblies of God (EAGT) ambayo hasara yake inakadiriwa kuwa zaidi ya Sh10 milioni.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top