Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MZUNGU WA TIMU YA SIMBA AWAKEJELI WANA YANGA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

MZUNGU wa Simba, Dylan Kerr amewakejeli Yanga kwamba wamewabahatisha wanachoonga, huku akiwatuliza mashabiki wa Mnyama kwamba wasipaniki mambo mazuri yanakuja, waache Jangwani wabwabwaje tu.

Kerr alisema kwa sasa hatatazama Yanga inafanya nini bali ataweka nguvu kuhakikisha timu yake inashinda mechi zake zote saba zilizosalia kabla ya mapumziko ya Ligi Kuu Bara mwezi Novemba ili waweze kuwa vizuri katika kuwania ubingwa.

Kocha huyo Mzungu kutoka Uingereza alisema mbali na kwamba walipoteza mchezo huo timu yake bado ni bora na inaweza kupata matokeo katika mechi zinazofuata hasa dhidi ya Stand United, mechi itakayopigwa keshokutwa Jumatano.

“Kwa sasa sitaki kutazama Yanga wanafanya nini, nitakwenda na takwimu kuhakikisha tunashinda mechi zetu zilizosalia ili tuweze kuwa pazuri.

“Tutaanza na mechi hizi saba za kwanza kabla ya ligi kwenda mapumziko, Yanga pia anaweza kushinda zote lakini hiyo haitatuhusu sana,” alisema Kerr.

“Timu yangu ni nzuri na inacheza vizuri, inanipa matumaini kuwa tunaweza kufanya makubwa, sina wasiwasi na kupoteza mchezo huo mmoja ambao pia tulicheza vizuri.”

BARTHEZ ALIKOMA KUMBE

Kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ amekuwa muwazi na kukiri kuwa washambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza na Mussa Hassan ‘Mgosi’ walikuwa mwiba kwao na kama mabeki wake wangezubaa basi wangekuwa wanazungumza mambo mengine.

Barthez ambaye amewahi kuidakia Simba kabla ya kujiunga na Yanga alisema safu yake ya ulinzi ilifanya kazi nzuri kuwadhibiti wawili hao vinginevyo wangefunga mabao kwenye mchezo huo.

“Niwe muwazi tu, Kiiza na Mgosi walikuwa hatari, walionekana kusaka ushindi kwa udi na uvumba, kilichosaidia ni kwamba safu yangu ya ulinzi ilikuwa imara vinginevyo mambo yangekuwa mengine, walikuwa mwiba sana kwetu.

“Kikubwa ni kwamba timu yetu imejipanga vizuri na inasaka ushindi katika michezo yote, hicho ndicho kilichotupatia ushindi katika mechi hiyo,” alisema.

Yanga na Simba zilicheza juzi Uwanja wa Taifa katika mechi iliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top