Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mamia ya wafungwa katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha watu kupoteza maisha.
Baada ya Dereva wa Taxi muumini wa dini ya kiislamu kuuawa, mapigano yalizuka siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.
Wafuasi wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina anti-balaka walishambulia gereza siku ya jumatatu, na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na wanamgambo.
Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu kundi la waasi wa kiislamu, Seleka kuchukua madaraka mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadae liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.Maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao.
Tangu machafuko mapya kuanza wikiendi, zaidi ya watu 30 wameuawa.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema watoto watatu waliuawa na mmoja kwa kuchinjwa.
Shirika la habari la AP limesema Watu 500 wametoroka gereza la Ngaragba lililopo mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui siku ya jumatatu jioni.
Rais wa mpito wa nchi hiyo Catherine Samba Panza amelazimika kukatiza safari yake ya kuelekea kwenye Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa.
Uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, mwezi mmoja kabla Baba Mtakatifu Francis kutembelea Bangui.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.
Filed Under:
KIMATAIFA
on Tuesday, September 29, 2015