MTANZANIA
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, limesema haliwezi kutaja bei rasmi ya gharama za umeme wa gesi hadi mtambo utakapoanza kufanya kazi ili kubaini halisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felchesmi Mramba
alisema Tanzania ni nchi ambayo inatumia kiwango cha chini cha gharama
za umeme ikilinganishwa nan chi jirani za Afrika Mashariki.
Alisema mitambo ya umeme wa mafuta
inatarajia kuzima ifikapo Septemba ndio maana wamesaini mkataba wa miezi
mitatu kwa vile mwezi huo ndio mradi wa umeme wa gesi unakamilika.
Alisema mitambo ambayo haitakatishwa mikataba ni ule wa IPTL na Nyakato.
“Mkataba
wa shirika la umeme IPTL ni wa muda mrefu hivyo hatuwezi kukatisha
mkataba isipokuwa tutaiomba ibadilishe mfumo na kutumia gesi lakini wa
Nyakato ni kwa kwetu” Mramba.
Alisema Serikali pia inafanya juhudi za
kupunguza utegemezi wa mitambo ya kufua umeme wa na kutumia mafuta
ambayo ni ghali zaidi na kuamua kutekeleza mradi wa Kinyerezi wenye
uwezo wa kuzalisha MW 150 ambao utagharimu zaidi ya bilioni 293 na
utakamilika Agosti mwaka huu.
NIPASHE
Mchakato wa kumpata mgombea urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeendelea kuibua mapya na kuleta
mvutano baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya,
kunukuliwa akisema kuwa majina matano yaliyopelekwa kwenye Kamati Kuu
ya CCM (CC) kutoka kwenye Kamati ya Maadili yalijulikana hata kabla ya
kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
Prof. Mwandosya ambaye ni Mbunge wa
Rungwe Mashariki amenukuliwa akisema hayo kwenye sauti yenye maelezo
yake iliyorekodiwa na kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Prof. Mwandosya alisema amepata taarifa za kusambazwa kwa sauti hiyo lakini hafahamu kama yanayozungumzwa humo ni ya kwake.
Prof. Mwandosya alisema anachokumbuka
akiwa kijijini kwao Lufilio wilayani Rungwe aliitwa na wazee na kufanya
nao mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kilichojiri wakati wa mchakato
wa kumpata mgombea urais CCM.
“Niliitwa
na wazee kwenye mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kimetokea na
inawezekana yaliyomo ndani ya hiyo clip yana ukweli, lakini wewe
unadhani nilichokisema ni uongo?, Si kinalingana na hali halisi
ilivyokuwa Dodoma,” alisema.
Hata hivyo, alisema taarifa zilizosambazwa kwamba anataka kuhamia Chadema siyo za kweli. Katika sauti iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Prof. Mwandosya
amenukuliwa akisema kuwa majina ya makada walioingia tano bora katika
kinyang’anyiro cha urais yaliyopelekwa Kamati Kuu yalijulikana hata
kabla ya kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
Alisema Mwenyekiti wa Kamati Kuu, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa na majina yake matano mfukoni na kamati yenyewe pia ilikuwa na majina yake.
Akizungumzia madai hayo, Prof. Mwandosya
alithibitisha kuwa madai hayo ni ya kweli na kwamba wajumbe wote wa
Mkutano Mkuu wa CCM waliokuwapo Dodoma wanalijua hilo.
“Hapo
mimi sioni kwamba kuna jambo ambalo limepotoshwa, kwani yote
yanayosemwa ni ya kweli na hata wajumbe wote waliokuwa Dodoma kwenye
Mkutano Mkuu wanayajua vizuri mambo hayo,” Prof. Mwandosya.
Alisema ingawa hajaisikia sauti
inayodaiwa kuwa ni yake, lakini kama ni suala la kusema kuwa mgombea
urais mteule wa CCM, Dk. John Magufuli hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa
tawi la CCM ni kweli.
Alizidi kueleza kuwa, anaona ni sahihi
kwa sababu katika kumbukumbu zake hajawahi kusikia wala kumwona Dk.
Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Chama katika ngazi yoyote.
“Nina
kazi nyingi sijafungua mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kidogo,
lakini kama mambo yanayosemwa ni hayo, sioni kama kuna uongo ndani yake,
ningepata shida sana kama mambo yanayozungumziwa yangekuwa siyo ya
kweli, katika kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Dk. Magufuli amekuwa
Mwenyekiti wa Chama au Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama, lakini sasa
ndiye atakayekuwa mwenyekiti wa Chama chetu nadhani hilo liko wazi,” alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Waziri Mkuu
aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Prof. Mwandosya alisema kuwa Lowassa ametumia haki yake ya
kidemokrasia na yeye haoni kama kwa uamuzi huo amefanya kosa lolote.
Alisema vyama vya siasa ni sawa na
madhehebu ya dini, ambapo waumini wanayo haki ya kwenda kuabudu katika
kanisa wanalolitaka au ambalo imani yao inawatuma na hakuna mtu wa
kuwapokonya haki hiyo.
“Alichokiamua
Lowassa sidhani kama ana kosa, kwani anayo haki na uhuru wa kufanya
alichokifanya, siku hizi kuna makanisa mengi, mtu anapoamua kwenda
kuabudu katika kanisa analoona linamfaa huwezi kusema kuwa amekosea,
labda ninachoweza kushauri ni CCM kujiuliza sababu za Lowassa kuondoka
na ikiwezekana ijisahihishe ili watu wengi zaidi wasiondoke,” alisema.
NIPASHE
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai
amehojiwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumshambulia
kwa fimbo na kumjeruhi mgombea mwenzake katika mbio za kuwania ubunge wa
Jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM, Dk. Joseph Chilongani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema kuwa walilazimika kumhoji Ndugai baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na tukio hilo lililotokea wilayani Kongwa juzi.
Inadaiwa kuwa Ndugai alimpiga fimbo na
kumjeruhi vibaya Chilongani wakati wagombea hao na wenzao watano
wanaowania kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM
walipokuwa wakijinadi ili wapitishwe na wanachama wenzao jimboni humo.
“Tulipokea
malalamiko, tumemhoji Ndugai na kisha tukamuachia kwa dhamana… hivi
sasa tunaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo,” alisema Kamanda Misime na kuongeza kuwa watatoa taarifa zaidi pindi uchunguzi ukikamilika.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya, alithibitisha vilevile kuwa Dk. Chilongani alipokewa kwao juzi jioni kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kongwa na kwamba hadi kufikia jana alikuwa bado akiendelea na matibatu.
“Anaendelea na matibabu lakini hali yake inaendelea vizuri,” Dk. Mpuya.
Dk. Chilongani, alisema kuwa juzi,
wagombea wote saba walifanya kampeni katika kata tatu na kabla
hawajamalizia ngwe hiyo, ndipo sakata hilo lilipozuka.
Aliongeza kuwa wakati wakimalizia
kujinadi kwenye kata ya Ugogoni, yeye alipanda jukwaani kujinadi kabla
ya kufuatiwa na Ndugai, kwa mujibu wa ratiba waliyopangiwa na kiongozi
wa msafara huo.
Alisema Ndugai baada ya kupanda
jukwaani, licha ya kunadi sera, alianza kumshambulia (Ngatunga), kwa
maneno makali akimtuhumu kuwa amekuwa akishirikiana na watendaji wa
halmashauri ya wilaya kufanya ubadhirifu.
“Aliposhuka
jukwaani, akaendelea kunishambulia kwa maneno, nikamwambia kwa hadhi
yako haustahili kufanya siasa za namna hii; akatishia kunipiga,”Ngatunga.
Alisema Ndugai kwa kutumia fimbo kubwa
aliyokuwa nayo mkononi muda wote, alimpiga Ngatunga kwenye paji la uso
na sehemu nyingine za mwili hadi akazimia.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies