Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA ZOTE NIMEKUWEKEA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
HABARILEO

Ikiwa zimebakia siku mbili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kieletroniki (BVR) kuisha, wengi wameiomba Serikali kuongeza muda wa kujiandikisha ili watu wengi wasiachwe bila kuandikishwa.



Imebainika pia kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka katika vituo vya BVR, tofauti na ilivyokuwa awali.Katika vituo kadhaa katika manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni, kulikuwa na idadi kubwa ya watu katika vituo vya kujiandikisha, licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuongeza mashine katika maeneo ambayo yana wakazi wengi.



Kutokana na siku za kuandikisha kufika ukingoni, wananchi wengi wameonekana kujitokeza na kuwa kwenye misururu mirefu. Wengine wameweka kambi katika vituo ili kuhakikisha wanapata fursa hiyo muhimu, huku wengi wakilalamikia kutoandikishwa licha ya kufika vituoni kwa takribani kati ya siku mbili au tatu bila kuandikishwa.



Katika Kituo cha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo eneo la Mabibo, kulikuwa na umati wa wananchi wakiwa wameketi chini huku wengine wakionekana kukata tamaa, hasa kutokana na wengine hata kutopewa namba au kuandikishwa majina yao.



Awali zilikuwepo mashine nne, lakini sasa zimeongezwa na kufikia 12. Pamoja na Tume kuongeza mashine, bado idadi ya watu wanaojitokeza imezidi kuongezeka. Katika kituo cha Shule ya Msingi Msewe, idadi kubwa ya wananchi walionekana kupiga kambi bila kukata tamaa.



Aidha, Ofisa kutoka Tume, Gudluck Msomigulu anayesimamia vituo vilivyopo eneo la Shule ya Msingi ya Mlimani, alisema pamoja na kuongezewa mashine na kufika nne, bado wameelemewa na idadi ya watu wanaojitokeza kila siku.

Katika kituo kilichopo eneo la Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam( UDSM) ukumbi wa Nkurumah, kulikuwepo msururu mkubwa wa watu waliokuwa wakisubiri kuandikishwa, ilhali kukiwa na mashine moja.



HABARILEO

Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini Tanzania.



Baada ya kuitumikia nchi kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa Rais wa Awamu ya Tano mara baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.



Kutokana na kuheshima Katiba na kuendesha kwa ufanisi mchakato wa kumpata mrithi wake kuanzia ngazi ya chama tawala, CCM, Abbot amesema; “Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani namna hii.’’



Aidha, Abbot alimtaka Rais Kikwete awe na uhakika kuwa “ Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza uchumi.”



Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii. Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia, Peter Cosgrove.



Alipokelewa jana katika makao Makuu ya kiongozi wa Australia kwa heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na baadaye kupanda mti kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.



Tanzania na Australia zimedumu katika ushirikiano baina ya nchi zao tangu miaka ya 1960 na sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.



Baadaye jana, Rais Kikwete alitarajiwa kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika kutokana na kupata gesi.



Tayari Serikali ya Australia na kampuni binafsi za gesi na mafuta, zinaisaidia Tanzania hasa katika Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) na tafiti mbalimbali katika Kilimo.



Leo, Kikwete anatarajiwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla. Mara baada ya kupokea shahada yake, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania.




NIPASHE

Kampeni za ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mtera, Dodoma zimeingia dosari, baada ya kuzuka vurugu za vijana wanaodaiwa kuwa wapambe wa Mbunge anayemaliza muda wake, Livingstone Lusinde, kufanya fujo wakati wa kunadi wagombea.



Tukio hilo lilitokea juzi wakati wagombea ubunge kupitia chama hicho wakiwa katika kampeni za kujinadi kwa wapigakura wa kwenye kijiji cha Manzase, wilayani Chamwino.



Inadaiwa kuwa vijana hao wanaodaiwa kuwa sio wakazi wa kijiji hicho walipelekwa kwa magari matatu aina ya Fuso na kuanzisha vurugu baada Lusinde kumaliza kujinadi kwa wapigakura na kuwataka vijana hao kuanza kuzomea mgombea atakayepanda jukwaani kujinadi.



Baada ya kushuka mbunge huyo ndipo vijana hao walipoanzisha vurugu zilizovuruga mkutano huo na baadhi ya wagombea kukosa nafasi ya kujinadi.

Kutokana na vurugu hizo,  wagombea tisa waligoma kuendelea na kampeni hadi kiitishwe kikao kitakacho jumuisha wagombea wote ili kujadiliana na viongozi wa chama na kutoka na maazimio.



Kikao hicho kilifanyika jana asubuhi chini ya Katibu wa mkoa, Alberth Mgumba, na kuelekeza kusogeza muda wa kuanza kampeni hizo.

 Wagombea wakitakiwa kuondoka saa mbili asubuhi, lakini walianza kuondoka kuelekea vijijini saa tano.



Katika kikao hicho wagombea wote tisa kati ya kumi walimlalamikia Lusinde kwa Mbungu kwamba aliwatumia kuwatumia vijana kufanya fujo ili  kuharibu mikutano mara anapomaliza kuwahutubia wananchi.



“Nani asiye jua kuna vijana kama wale wa jana (juzi) sio wakazi wa eneo lile, lakini walikuwapo kwenye mkutano ule na ndio walikuwa mstari wa mbele kuharibu mkutano huo kwa kufanya fujo na kuzomea wagombea wengine,” alisema mmoja wa washindani wakubwa wa Lusinde.



Wagombea wote waliazimia kuwa katika mikutano iliyobaki katika vijiji mbalimbali wakikutwa watu ambao si wakazi wa eneo husika inabidi waondolewe na polisi kudhibiti uwezekano wa kuvuruga mikutano ya kampeni.

Mgumba alisema kuwepo kwa changamoto katika mikutano kampeni ni jambo la kawaida kwa kuwa kila mgombea ana tabia zake, hivyo hawawezi kufanana na kwamba changamoto hizo zitatatuliwa ndani chama.



NIPASHE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeongeza saa za kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) mkoani Dar es Salaam kutoka saa moja asubuhi badala ya saa mbili ya sasa hadi saa 12 jioni.



Tume imesema hatua hiyo imefuatia malalamiko ya wakazi wa mkoa huo kuwa baadhi ya vituo vinachelewa kufunguliwa na kufungwa mapema.

Kadhalika NEC imesema idadi ya waliokwishaandikishwa kwenye daftari hilo hadi juzi jijini humo, imefika 1,172, 855 kwa Kinondoni watu 490,228, Temeke 389,558 na Ilala 302, 871.



Pia jumla ya mashine za BVR ambazo hadi sasa zitatumika katika uandikishaji katika jiji hilo ambalo ni mkoa wa mwisho katika kazi hiyo ni 3,717 kwa Ilala yenye vituo 395, ina BVR 927 sawa na asilimia 117, Kinondoni yenye vituo 702, BVR 1462 sawa na asilimia 104 huku Temeke yenye vituo 572 ikiwa na BVR 1,328 sawa na asilimia 116.



Hata hivyo, NEC imesema mashine hizo zinatarajiwa kuongezwa kadri ya uhitaji wake kwenye vituo vya kujiandikisha.



Baada ya kukutana na uongozi mzima wa Mkoa wa Dar es Salaam kujadili uandikishaji huo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema vituo vya kujiandikisha vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.



Alisema kwa sasa tume hiyo haiwezi kuzungumza iwapo imeongeza muda, lakini itahakikisha watu wote waneandikishwa mkoani humo. Jaji Lubuva aliongeza kuwa maofisa uandikishaji wote wasio na uzoefu wa kutosha kwenye vituo wataondolewa na kutaka makundi maalumu wakiwamo wazee, wajawazito wapewe kipaumbele.



JAMBOLEO

Mapadri watatu na mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge wilayani Ngara walifariki dunia jana papo hapo huku watu 13 wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani wakiwahi Karagwe kwenye misa ya shukrani ya mwenzao aliyepata daraja hilo hivi karibuni.



Tukio lingine ni la juzi ambapo watu saba walikufa na wengine 44 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi na treni ya mizigo mkoani Tabora. Ajali hiyo ya juzi watu wanne walikufa papo hapo huku wengine wakifia njiani wakipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.



Katika tukio la kwanza la Ngara, kwa mujibu wa mmoja wa mapadri waliokuwa katika msafara huo, Erasto Nakule, ajali hiyo ilitokea jana saa 2:00 asubuhi katika barabara iendayo nchi jirani ya Uganda katika eneo la Bugorora wilayani Missenyi mkoani Kagera.



Alisema gari aina ya Land Cruser lenye namba ya usajili T.650 BY1 la Jimbo Katoliki la Rulenge lililokuwa likiendeshwa na Padri Florian Tuombe ambaye pia amefia katika Hospitali ya Mkoa Kagera liligongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya Sabuni lenye namna ya usajili T.166 AGU.



Alisema basi la Sabuni lilikuwa likitoka wilayani Karagwe kwenda mkoani Mwanza, ambapo Land Cruser ilikuwa ikitoka Biharamulo kwenda Karagwe.

Padri Nakule aliwataja mapadre waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na Michael Mwelinde (70), Onesmo Buberwa (40) na Florian Tuombe aliyekuwa dereva na Mtawa Magreth Kadebe (60).



Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa mapadri hao walikuwa ni walimu wa Seminari ya Rutabo wilayani Muleba na kwamba walikuwa wakienda kwenye misa ya shukrani ya Padre Evisius Shumbusho inayofanyika nyumbani kwao Karagwe.



Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo chake ni dereva wa Land Cruser kuendesha bila kuchukua tahadhari hivyo kugongana uso kwa uso na basi la Sabuni.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top