Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Bwana Salim Chima akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote walioshiriki katika Seminas hiyo.
Na Victor Mariki - Ofisi ya Makamu wa Rais
Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani ya asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania imeathirika na janga la ukame ambao unaweza kupelekea uzorotaji katika ukuaji wa uchumi na hata kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai.
Hayo yalielezwa na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Zainab Shaban Bungwa wakati akitoa mada katika semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira kwa watendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo leo.
Aidha Bi Bungwa alifafanua kuwa uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa rasimali asili kama vile ardhi, misitu, wanyamapori na maji ambapo inakadiriwa asilimia 75 ya wanachi waishio vijijini hutegemea zaidi ardhi katika uendeshaji wa maisha yao.
Pia aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imechukua hatua mbali mbali katika kukabiliana na janaga hilo kwa kuunda sera, mikakati na sheria mbalimbali za kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.
Baadhi ya mikakati, sera na sheria hizo ni Mkakati wa Hatua za Haraka Kuhifadhi Mazingira na Vyanzo vya Maji, Mkakati wa Bahari na Mabwawa, Program za Kupambana kwa Kuenea Hali ya Jangwa na Ukame, Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Program na Miradi inayotekelezwa na Sekretarieti ya Mikoa katika suala la Utunzaji Mazingira.
Sanjari na hayo Bi Bungwa alienda mbele zaidi kusema kuwa hivi sasa robo ya dunia ipo hatarini kukumbwa na hali ya jangwa kwa kuwa zaidi ya hekta bilioni 3.6 za ardhi yake tayari zimeshaathiriwa na janga hilo ambalo mpaka sasa limeathiri zaidi ya watu milioni 900 duniani kote .
Kwa upande wa bara la Afrika hivi sasa hali hiyo ya jangwa imekuwa ni tatizo sugu kwakuwa mpaka sasa tayari asilimia 73 ya ardhi yake imeshathirika vibaya na janga hilo hali ya jangwa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.