Featured

    Featured Posts

Loading...

CHAKUFANYA PINDI SIMU IKIDONDOKA KWENYE MAJI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Wengi  kwa sababu mbalimbai tumewahi kudondosha simu kwenye maji. Kwa watumiaji wa simu kudondosha simu ni suala la kawaida.

Kwa wengi baada ya kitendo hiki huwa tunajaribu kutafuta njia mbalimbali za kuokoa simu zetu ili zisiharibike zaidi.

Katika makala haya nitajaribu kutoa maelezo mafupi ya nini cha kufanya ikiwa simu yako imedondoka kwenye maji ili isiweze kupata madhara zaidi na uweze kuokoa taarifa ulizohifadhi kwenye simu hiyo.

Kwa hali ilivyo inawezekana simu kama kifaa isiwe tatizo pale inapodondoka, lakini muhimu ni zile taarifa zilizomo ndani ya simu.

Kuna uwezekano kwamba simu yako ilikuwa imewaka wakati inadondoka kwenye maji, kama maji yakiingia ndani mfumo wa umeme unaweza kuharibika kwa kupiga shoti. Sasa fuata hatua hizi

Zima simu yako. Ukishazima hatua muhimu inayofuata ni kutoa vitu vyote kwenye simu kama betri, kasha, kadi na vitu vingine ambavyo vinatumika kwenye matumizi ya simu yako.

Itingishe. Tingisha simu yako juu na chini hasa sehemu za kuingiza umeme au kuchomeka kifaa cha kutoa picha au video au kifaa cha kuchomeka visikilizio na sehemu za kubonyeza.

Baada ya kutingisha tumia kitambaa laini , pamba au sponji kukausha maji yaliyopo kwenye simu yako kama yaliingia.

Iweke ndani ya mchele. Kama una mchele kwenye mfuko au chombo maalumu, iweke simu yako halafu funika kisha weka kwenye sehemu iliyokauka hii itasaidia kunyonya maji maji na mengine kwenye kifaa chako .

Acha simu yako ndani ya mchele kwa saa 24 mpaka 48, usijaribu kuiwasha au kuishika muda wote huo kuona kama imeanza kufanya kazi au la. Kama haikuwa na maji mengi ndani ya muda huo, itaanza kufanya kazi.

Weka akilini kwamba si lazima simu yako iwake baada ya kufanya yote hayo, kuna uwezekano wa asilimia 50 tu  wa simu yako kuwaka na kufanya kazi tena.

Peleka kwa mtaalamu. Kama imeshindikana kuwaka baada ya jitihada zote hizo ni vizuri upeleke kwa wakala aliyeidhinishwa  kuuza au kutengeneza simu husika kama umenunua kwake

Pamoja na maelezo yote hapo tu, unatakiwa ujiandae na ujue njia za kuikinga simu yako dhidi ya maji siku nyingine.
Kama unatembea sehemu za mvua au maji maji kama baharini, mto au bwawani unaweza kununua mfuniko usioingia maji kwa ajili ya kukinga simu yako

Mifuniko hii ina sehemu unayoweza kuangalia kama kuna simu imeingia, ujumbe au kitu kingine.

Suala la simu yako kuingiliwa na maji au kupata tatizo la umeme, mara nyingi halipo kwenye ‘warranty’  ili kuweza kupata faida ni bora kuwa na bima ya simu na vifaa vingine vya elekroniki ili inapopata shida iwe rahisi kupata nyingine kuliko kutumia gharama kubwa kununua kifaa kingine.

Muhimu ni kujua na kuzingatia suluhisho hili. Lakini njia nzuri zaidi ni kupeleka simu yako kwa fundi au mtaalamu wa simu ili aweze kuingalia na kufanya marekebisho kama kuna uwezekano huo.

Kuendelea kutumia simu mbovu au zenye shida fulani zinaweza kukuletea madhara ya kiafya, kwa sababu kuna vifaa ndani ya simu vinaweza kufanya kazi ndivyo sivyo. Vifaa hivi ni kama  kioo, mfumo wa sauti na mfumo wa umeme. Natoa tahadhari kwa watumiaji wa simu wenye mazoea ya kuchokonoa vifaa hivyo pasina ujuzi wowote. Hiyo ni kazi ya fundi.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top