Watu wapatao watano kutoka mkoani Shinyanga wametiwa mbaroni kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya viungo vya binadamu.
Bwana Justus Kamugisha ambaye ni kamanda wa police mkoani Shinyanga amesema mnamo tarehe 21st May 2015 majira ya saa saba mchana huko kahama mjini katika hotel maarufu kama Maji hotel walifanikiwa kuwakamata watu watano ambao majina yao nikama ifuatavyo.
1. Bahati kirungu umri wake ni miaka 56 kabila msukuma pia ni mwalimu wa shule ya msingi Katunguru iliyopo tarafa ya msalala wilaya ya kahama.
2. Muoja John umri wake ni miaka 24 kabila msukuma yeye ni mkulima nanimkazi wa isagei wilayani nzega.
3. Bilia Busana umri wake ni miaka 39 kabila msukuma yeye ni mkazi wa moga Nzega
4. Shija Makandi (mwanamke) umri wake ni miaka 60 kabila msukuma na mkazi wa lusagerwa wilayani nzega Tabora
5. Regina Kashinje umri wake ni miaka 40 kabila msukuma huyu ni mkulima pia ni mkazi wa insagee wilayani nzega mkoani tabora.
Watu hawa walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kuuza viungo hivi vya binadamu kwa mtu mmoja kwa thamani ya Tsh 600 millions. Endelea kutembelea Mutalemwa Blog.