Mtoto mmoja aliingia saluni ya mtaani kwao, baada ya kuingia saloon hapo kinyozi akamnong’oneza mteja wake, kaka unamuona huyo mtoto aliyeingia hapa ndani, mtoto huyu ni mbulula hakuna mfano.
Angalia, ngoja nikuhakikishie kwamba mtoto huyu ni Ziro kabisa. Kinyozi akachukua noti ya shilling 2, 000/= akaiweka upande mmoja wa meza na akachukua tena noti ya shilling 1, 000/= akaiweka upande mwingine wa pili mwa meza.
Akamuita yule mtoto akamwambia unataka ipi kati ya hizi noti mbili? Mtoto akanyonya kidole kisha akachukua noti ya shilling 1, 000/= kisha akaondoka zake. Kinyozi akamwambia yule mteja wake, umeona? Mara zote mtoto huyu ndo hivyo afanyavyo, hajifunzi kabisa wala ajui ipi ni pesa kubwa kubwa ipi ndogo, Ziro kabisa.
Baadaye yule mteja akaondoka saluni hapo, katika pitapita zake mtaani akakutana na yule mtoto analamba ice cream, akamuuliza, hivi kwa nini uliamua kuchukua noti ya shilling 1,000/= na ukaacha kuchukua noti ya shilling 2, 000/=?
Mtoto akamjibu yule mteja ivi, siku nikichukua noti kubwa, yule kinyozi atajua nimeanza kuwa na akili na mchezo wa kufaidi hela zake utakuwa umekwisha, kwaiyo we muache aendelee kuniona mbulula nifanye yangu.
Swali kwako msomaji wangu, ivi unafikili kati ya kinyozi na huyu mtoto nani anastahili kuitwa mbulula? Endelea kutembelea Mutalemwa Blog
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.