Jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa baadhi ya Madereva wa mabasi yanayosafirisha abiria kwenda mikoani na nchi Jirani kutokana na madereva hao kuwachagulia abiria maeneo ya kula chakula na kujisadia tabia ambayo imeelezwa kuendelea kuwa sugu kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa abiria kila siku.
Kutokana na tabia hiyo abiria wametakiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ikiwemo askari wa usalama Barabarani pindi Dereva anapokuwa mkorofi kwa abiria wito ambao umetolewa na mkuu wa elimu kwa umma kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu wa polisi bwana abed swai wakati akiongea na ITV jijini Dar es Salaam.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.