Kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari na mitandaoni pia kwamba Serikali ilikuwa na mpango wa kuiondoa Jamii ya Wamasai katika eneo la Loliondo, ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu aliwahi kukanusha juu ya hilo siku tatu zilizopita.
Jana kupitia ukurasa wa Twitter, Rais Kikwete ameandika kwamba Serikali haina mpango na wala haitowatoa Wamasai kutoka katika ardhi hiyo ambayo ni urithi wa mababu wa jamii hiyo.
Ujumbe aliouandika Rais kupitia ukurasa wake wa Twitter jana Novemba 23 unasomeka hivi; “…There has never been, nor will there ever be any plan by the Government of#Tanzania to evict the #Maasai people from their ancestral land…“– @jmkikwete
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.