Chama cha wananchi CUF leo hii kimewataka waziri mkuu mhe.Mizengo Pinda, mwanasheria mkuu jaji Fredrick Werema, waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo, pamoja na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini mhe.Eliakim Maswi kuachia ngazi mara moja au kufukuzwa kazi kutokana na na wao kuonekana wazi kuwa wanatetea ufisadi wa mabilioni ya Esrow.
Profesa Hibrahim Lipumba amesema kuwa viongozi hawa wamekuwa mstari wa mbele kuonesha wazi kuwa hawako tayari kuona wahusika wa ufisadi huo wakiadhibiwa hivyo hawana sifa ya kuendelea kuiongoza nchi kwani hawana maslahi kwa wananchi, huku akiitaka Takukukru nao kuwachunguza viongozi hao kama wanausika na ufisadi huo wa ishu ya account ya Tegeta Escrow.
Hivi karibuni tulimsikia waziri mkuu akijaribu kuwadanganya wanachi kuwa fedha zilizopo kwenye account ya tegeta Escrow sio mali ya umma bali ni mali ya kampuni binafsi, amesema Lipumba leo. Pia CUF imewataka Takukuru kuwakamata vigogo kama James Rugemalira pamoja na Harbinder Singh Seth na kuwafungulia mashtaka ya rushwa na wizi wa mali za Tanesco kwani hawa ndio wahusika nambali moja waliozigawa pesa hizo kama za kwao.
Lipumba ametaka pia mkurugenzi wa tanesco pamoja na bodi nzima ya tanesco kufutwa mara moja kwa kuwa haikutimiza wajibu wake wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza. Lipumba amesema chama chake kitafanya maandamano ya nchi nzima baada tu ya mjadala huo kumalizika bungeni kuwashinikiza viongozi waliohusika kuwajibishwa na pia kuwapongeza wabunge waliosimamia kufichua ufisadi huo.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.