Watu wapatao 16 wamedhibitika kuugua ugonjwa hatari wa Rubella, ugonjwa usio kuwa na tiba, na ugonjwa huu una ambukiza kwa njia ya hewa.
Na wakati huo huo watu wapatao wanne wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Surua kati ya sampuri 55 zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa mbalimbali walio hisiwa kuugua ugonjwa wa Surua.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza mwandisi Bw. Evarist Ndikilo, alitoa takwimu hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni shilikishi ya chanjo ya surua Rubella iliyofanyika kimkoa katika zahanati ya Kirumba jijini Mwanza, ambapo amesema manispaa ya Ilemela ndio inayo ongoza kuwa na wagonjwa wengi wa ugonjwa wa Rubella ambapo idadi yao ni 11, huku takwimu zikionesha kupungua kwa ugonjwa wa Surua na kufikia idadi ya wagonjwa 4 katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi mwezi June mwaka huu.
Utafiti wa maambukizi ya ugonjwa wa Rubella uliofanywa na madaktari wa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza umebaini kuwa wajawazito 317 sawa na 92.7% (asilimia) kati ya wajawazito 342 walisha wahi kuugua ugonjwa huo nakupata kinga, lakini wajawazito 25 ambao ni sawa na 7.3% (asilimia) hawakuwa nakinga yoyote dhidi ya ugonjwa wa Rubella, ivyo walikuwa wako kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye madhala ya Rubella endapo wataambukizwa ugonjwa huo.
Mkoa wa Mwanza katika kampein hiyo ya siku 7 unatarajia kuwapatia chanjo watoto zaidi ya 1.300,000 (million moja na laki tatu), wenye umri kuanzia miezi 9 hadi chini ya miaka 15 dhidi ya surua rubella, matone ya vitamin A na dawa za kuuwa minyoo.
Kumbuka kampeni ya chanjo ya Surua Rubella kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi miaka 15 itadumu kwa kipindi cha siku 7 tu ambapo imeanza rasmi tarehe 18/10/2014 na itamalizika siku ya tarehe 24/10/2014, na chanjo hii itatolewa bila malipo yoyote.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO >> MUSIC MPYA