Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MLIPUAJI WA MABOMU MKOANI ARUSHA AULIWA NA POLISI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio hayo.

Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Akitoa taarifa za kifo cha mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha Lebaratus Sabas amesema marehemu yahaya hassan omari hela maarufu kwa jina la (sensei) ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikamatwa wiki mbili zilizopita mkoani morogroro na kupelekwa arusha na bado alikuwa anaendelea kuhojiwa.

Kwa mujibu wa kamandaa sabas mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa marehemu yahaya, alikiri kuwa yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa matukio yote ya milipuko ya mabomu na ya kumwagia viongozi wa dini tindikali yaliyowahi kutokea mkoani arusha na maeneo mengine.

Aidha kamanda Sabas Amefaanua kuwa baada ya marehemu ambaye ni mtuhumiwa kukiri tuhuma hizo alikuwa bado anaendelea kutoa ushirikiano kwa kuanza kuonyesha vitendea kazi yakiwemo mabomu ambayo alidaiwa kuyaficha kondoa mkoani Dodoma.

Amesema wakati anasafirishwa walipofika eneo la kisongo katika barabara kuu inayoenda dodoma majira ya usiku alifanya jaribio la kutaka kutoroka na ndipo akapigwa risasi iliyomjeruhi mguu na kiuno na akafariki wakati anapelekwa hosipitali.
  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top