Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANACHI WACHOMA BUNGE LAO MOTO KISA KATIBA MBOVU

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Wananchi wa nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa kukaa madarakani. Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo.

Taarifa kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress yamechomwa moto pia. Bunge hilo lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.

Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao. Kabla ya kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia waandamanaji waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani watu 1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.

Waandamanaji walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta huku magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.

Kwa picha zaidi juu ya tukio hili bofya hapa sasa>>

  


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top