Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MGONJWA WA EBOLA AHISIWA KUINGIA MKOANI KILIMANJARO

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
 Wakazi wa kata ya Shirimatunda katika maanispaa ya Moshi, wameingiwa na hofu ya kupoteza maisha yao,kufuatia taarifa za kuwapo kwa mtu anayedhaniwa kuwa na ugonjwa hatari wa Ebola anayehudumiwa katika zahanati ya kata hiyo.



Kutokana na hofu hiyo,halmashauri ya manispaa ya Moshi imelazimika kuifunga kwa muda usiojulikana zahanati hiyo na kuwahamishia wagonjwa katika hospitali nyingine ikiwamo ya St Joseph katika manispaa hiyo.



Ripota wetu ambaye alikuwa eneo la zahanati hiyo alishuhudia baadhi ya madaktari wakiongozwa na mganga mkuu wa manispaa hiyo,Dk Christopher Mtamakaya pamoja na wataalamu wengine wa afya wakifanya kikao cha dharura kujadili hali hiyo.

Kadhalika,waandishi wa habari waliokuwepo katika zahanati hiyo walishuhudia baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa na mavazi rasmi yanayotumiwa na madaktari wanaohudumiwa wagonjwa wa Ebola.

Pamoja na kikao hicho,Zahanati hiyo imewekwa tangazo katika lango kuu linalosomeka 'Huduma zote za afya zimesitishwa kwa muda, Utawala' hali ambayo imeendelea kuzua maswali mengi kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu katika zahanati hiyo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kigongoni,kata ya Shirimatunda ilipo zahanati hiyo,Juma Sambeke alisema hajashirikishwa katika maamuzi ya kugeuza Zahanati hiyo kama Karantini ya mtu anayedhaniwa kuwa na Ugonjwa wa Ebola.

Alisema kuwapo kwa karantini hiyo kumeanza juzi majira ya saa 10 jioni baada ya kupokea taarifa kutoka afisa mtendaji wa kata hiyo kwamba zahanati hiyo itafungwa kwa muda ili kumhudumia mtu anayedhaniwa kuwa Ebola.















Lango kuu la kuingia zahanati ya Shirimatunda likiwa na tangazo la kusitishwa kwa huduma za afya katika zahanati hiyo kwa hofu ya kuwapo kwa mgonjwa wa Ebola.


"Manispaa haikuwa sahihi kuitumia zahanati hii kama karantini ya hofu ya Ebola, hapa kuna shule ya chekechea, sekondari, seminari ya Don Bosco na majirani kama unavyowaona....wasipopewa elimu na kama huu ni ugonjwa wa Ebola watu watakufa sana"alisema.


Sambeke alisema maeneo yatakayoathirika zaidi na kufungwa kwa zahanati hiyo ni Shirimgungani,Cherereni ya Moshi vijijini,Karanga, Soweto,Bonite madukani na mtaa wa Kigongoni ambapo zahanati huudumia zaidi ya watu 5,000 kwa mwezi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Shirimatunda,Felix Mushi alisema huduma za utoaji wa chanjo ya magonjwa ya Rubella na Surua zimehamishiwa katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo huku wagonjwa wengine wakihamishiwa maeneo mengine.

Alisema tarifa za awali alizopata ni kwamba mtu huyo alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), ambapo alisafirishwa hadi kwenye zahanati hiyo baada ya kudai kuwa na dalilizinazoashiria ugonjwa wa Ebola.

Aidha taarifa zaidi zinadai kuwa wataalam wamechukua sampuli kutoka kwa mgonjwa huyo kwa ajili ya vipimo, ili kujiridhisha, wakati huduma nyingine za matibabu zikiendelea kutolewa kwa mgonjwa huyo anayedaiwa kusafiri kutoka nchini Senegal.

Mmoja wa wakazi anayeishi jirani na zahanati hiyo, Thadei Sangawe,alisema ameanza kufanya mawasiliano na ndugu wengine waliopo maeneo mengine mkoani humo ili aweze kuhamisha familia yake kuepuka madhara kama ugonjwa huo utakuwa wa Ebola. 

"Tunaomba viongozi wenye dhamana hususani madaktari watoe taarifa kwa wananchi juu ya hii hofu iliyopo,maana kukaa kwao kimya kutasababisha wananchi washindwe kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha 
madhara"alisema.



Baadhi ya wagonjwa na wauguzi katika zahanati ya Shirimatunda wakihamia katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Shirimatunda kuendelea na huduma za tiba ikiwamo utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella.


Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Shaban Mtarambe, alisema hayuko tayari kuzungumza kwa maelezo kuwa suala hilo ni la kitaalam zaidi linalohitaji waataala wa kada ya afya kulizungumzia.


Naye mganga mkuu wa manispaa ya Moshi,Dk Christopher Mtamakaya alipohojiwa kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa mgonjwa huyo hakuwa tayari kuzungumza zaidi na alipotumiwa ujumbe wa simu ya mkononi alijibu kwa kifupi, huo ni Uvumi.

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa huo,Dk Mtumwa Mwako alipohojiwa kuhusiana na kuwapo kwa mgonjwa huyo naye alisema hafahamu na aliomba kupewa muda kwani alikuwa katika kikao.Kuhusiana na suala la mgonjwa huyo,katibu tawala wa mkoa huo, DkFaisal Isa alisema taarifa za kwanza anapata kutoka kwa mwandishi wetu na akaomba muda wa kufuatilia zaidi.

   



Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.

 FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO >>  MUSIC MPYA
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top