Wanafunzi walemavu Pongwe wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa vifaa vya kujifunzia, usafiri wa kuwawezesha kutoka shuleni kwao na kwenda sehemu mbali mbali za kujifunzia.
Pamoja na hayo wanafunzi hao wamesema kuwa ukosefu wa huduma za kijamii kama hospitali kutokuwepo karibu na maeneo ya shule yao nimoja ya jambo linalowatatiza sana, ambapo mwanafunzi anapoumwa nyakati za usiku walimu hulazimika kukodi pikipik maarufu kama bodaboda kwa ajiri ya kumpeleka mwanafunzi hospitalini.
Kwa sasa wanafunzi hawa wanalazimika kuishi kwenye bweni moja,kutokana na ukosefu wa mabweni ya kutosha, ambapo wanafunzi hawa wanaendelea kueleza kwamba umbali kati ya hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Mombo kuna umbali wa 12km, jambo ambalo linawapa hofu kubwa sana watoto wenyewe,wazazi pamoja na walezi wao.
Shule hii nishule yenye mchanganyiko wa watoto wenye uremavu wa aina mbali mbali, kama Albino, kutoona pamoja na kutosikia. Jamani kama wewe ndugu msomaji wa habari hii umeguswa na jambo hili ni wakati wako kuweza kutoa mchango wako ili kuiwezesha shule hii ya watoto wenye uremavu mbalimbali kuweza kujikwamua na matatizo hayayanayo ikumba kwa sasa.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO >> MUSIC MPYA