I.s.k & M.o.j.w. Campany limited press Tanzania,
Hostel ubungo,
S.L.P 1014,
Dar-es-salaam.
© Mutalemwa O. Juvenary 2010 na Aisha. S. Kiumwa
Mkaguzi: Rajabu.Hiteshi
ISBN 6375 7 10718
Toleo la kwanza 2011
MTUNZI:
AISHA SAIDI KIUMWA
Haki zote za kunakili zime hifadhiwa.Hairuhusiwi ama kuiga, kunakili,
kutafsiri, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila hidhini ya
I.s.k & M.o.j.w. Campany limited.
I.s.k & M.o.j.w. Campany limited.
Ilikuwa ni siku ya tarehe: 18/07/1990, siku yenye furaha na amani katika mji wa Karan nchi ya Kabanfu.Ni siku ya raisi wao bwana Shabibu mkewe alikuwa amejifungua mtoto mzuri wa kike, baada ya kukaa kwa muda wa miaka 15 katika ndoa yao bilakupata mtoto.Bwana Shabibu alikuwa hana nguvu za kiume( uwezo wa kuzaa ) alimtesa sana mkewe na kumwambia amzalie Mtoto.Bi Harisa yaani mke wa raisi Shabibu,alilia daima kwa mateso aliyopata.Siku moja Bi Harisa akawa anawaza juu ya mateso anayopata,akaamua kuzaa na mmoja wa watumishi wake pale kwake.Kulikuwa na watumishi wengi sana.Ilipofika usiku mumewe akawa amerudi,alimpokea kwa furaha sana.Lakini mumewe akamwambia:
Raisi Shabibu: Hivi wewe mwanamke unataka nikuuwe?
Bi Harisa: kwanini mume wangu?
Raisi Shabibu: Nimekwambia nataka mtoto,kwanini unizalii?
Bi Harisa: Mume wangu jua mtoto anatoka kwa Mungu.
Raisi Shabibu: Kelele wewe (Kwa ukali), pumbafu unakula bure, unalala
bure kuzaa hutaki.
Bi Harisa: (analia)
Siku iliyofuata raisi Shabibu akawa amepata safari ya kwenda nchi jirani,akamuaga mkewe.Akapanda ndege yake na kuondoka.Bi Harisa alipofika nyumbani akamwita mtumishi wake aitwae Kapona.Bi Harisa alitoka hadi nje,uku akimwita Yule kijana kwa sauti kubwa uku akisema.
Bi Harisa: Kaponaa!!!
Kapona: Ndio mama,
Bi Harisa: Njoo haraka ninashida na wewe.Kapona alikuwa na wasiwasi sana.Kwani tangu alipofika hapo akuwahi kuitwa na bi Harisa.Hivyo alijua kuwa lazima kafanya kosa.Basi akaondoka kumfuata bi Harisa wakaenda mpaka ghorofa ya juu sana.Huko Kapona hakuwahi kufika zaidi ya kuishia kupaona tu kwa macho.Huku watumishi wengine wakaanza kusema. “Duu! leo kapona kaenda juu sijui kuna nini” walisikika wakisema.Basi kule juu, bi Harisa akamwamuru Kapona akae kwenye kiti.Kapona akatii hamri ya bi Harisa.
Mara maongezi yao yakawa kama ifuatavyo:
Mara maongezi yao yakawa kama ifuatavyo:
Bi Harisa: Kapona nimekuita hapa nina shida na wewe, je upotayali?
Kapona: Shida gani hiyo mrembo wa bwana Shabibu!
Bi Harisa: Nadhani unajua kuwa nateseka sana kwa sababu sina mtoto.Bwana ananitesa.Naumia na nimechoka je unaweza kunisaidia?
Kapona: Nitakusaidiaje?
Bi Harisa: Si kazi kama hautojari! Naomba tuwe na uhusiano wa diri mimi na wewe, asijue mtu yeyote yule.
Kapona: Hapana! Naogopa wewe ni mke wa mtu tena ni mkubwa sana.
Bi Harisa: Najua ! lakini imenibidi,na ukini kubalia nitakupa kile
ukipendacho na pia nita kupandisha cheo.
Kapona: Hapana naogopa! Naogopa kabisa!
Bi Harisa: Nisaidie Kapona nakupenda sana!
Kapona: Sawa lakini nitakusaidia vipi?
Bi Harisa: Si nimekwisha kwambia yaani leo tulale wote.
Kapona: Hapana mimi siwezi kulala humu ndani.
Bi Harisa: Kwa sababu gani?
Kapona: Wenzangu watajua.
Bi Harisa: Sawa basi kesho tutatoka wote tutaenda hotelini kutembea.
Kapona: Sawa!!
Siku ya pili bi harisa akiwa chumbani kwake akijiandaa, akachukua kiasi kikubwa cha fedha na kuweka katika mkoba wake.Pia akakumbuka kuwa alisahau kanga.Akaludi ndani na kuichukua kanga hiyo na kutoka hadi nje na kumwita Kambona, na kumuuliza yuko wapi Kapona? Nimemuona anaelekea kule nje, akamwambia fanya haraka ukamwite.Alipoitwa Kapona bi Harisa akamuuliza “ulikuwa wapi wewe kipenzi changu cha moyo?” Kapona akajibu nilikuwa nafanya usafi kule nje ya geti.Bi Harisa akamwambia kuanzia sasa sitaki kukuona unafanya kazi yoyote.Haya jiandae tuondoke.Kapona akajibu sawa.Baada ya muda Kapona akatoka akiwa amevaa vizuri akapanda gari na safari ikaanza.
Dereva alikuwa bi Harisa mwenyewe.Kapona alipo jaribu kusema nikusaidie alikataa katakata.Kwenye gari waliongea maneno mengi sana.
Bi Harisa: Unajua kuwa nakupenda sana?
Kapona: Najua! Lakini hata mimi nakupenda.Je mzee akijua itakuwaje?
Bi Harisa: Usiogope mimi nipo na ananipenda sana.Mzee.
Kapona: Sawa. ILOVE YOU!
Ilipotimia majira ya saa 6:00 mchana.Bi Harisa na Kapona walikuwa wamewasili ndani ya hotel kubwa naya kifahari.Ilikuwa ni hotel ya KAPION ni hotel maarufu sana.Bi Harisa akashuka akiwa amevaa kanga na kujifunika mtandio mkubwa ilimradi asionekane.Mara akaingia tena kwenye gari na kumwambia Kapona.Chukua hela hii nenda kakodi chumba, alafu uje uniite.Kapona akashuka na kwenda moja kwa moja hadi mapokezi.
Muhudumu: Karibu, sijui nikusaidie nini?
Kapona: Naomba chumba.
Muhudumu: Nenda chumba namba 116 na ni shilingi elfu hamsini kwa siku.Kapona akatoa hela na kumpa Yule muhudumu.Harafu akaenda kumuita bi Harisa.Akashuka na wakaongozana moja kwa moja hadi chumbani.Walikula, wakanywa na wakatimiziana shida zao.
Nisaa 12:00 jioni ndipo bi Harisa akashtuka baada ya kutoka kwenye usingizi mzito na kumwamsha Kapona.Wakavaa na kuwasili kwao.Walipo fika, Kapona alikuwa ni mpole na mwenye hofu.Siku ya pili mzee Shabibu akawa amerudi,mkewe akawa amefurahi sana lakini Kapona alikuwa na wasi wasi.Ilipofika usiku mzee Shabibu akamwambia mkewe kuwa anahamu nayeye.Baada ya zoezi hilo wote wakalala wakaja kushtuka saa 4:00 asubuhi.Siku hiyo mzee Shabibu hakufanya kazi, alipumzika tu.Mara mzee Shabibu akasema nenda kamwite Kapona nina maongezi nayeye.Mkewe akatoka na kwenda kumuita.Kapona alipoingia akamsalimia bosi wake na akaambiwa kaa hapa.
Mzee Shabibu: Nafurahi, na ninakushukuru kwa kazi uliofanya.
Kapona: Kazi gani hiyo?
Mzee Shabibu: Umefanya vizuri sana, na ninakuhaidi nitakupandisha cheo kwa kuwa umenirindia nyumba yangu vizuri na kuanzia sasa wewe ni mkuu wa walinzi.
Kapona: Ahsante bosi na Mungu akubariki.
Kapona: Ahsante bosi na Mungu akubariki.
Bi Harisa alifurahi sana akasema “nilikwambia Kapona linda vizuri utapata zawadi yako umeiyona?” Kapona akajibu nakushukuru sana,nitafanya vizuri zaidi.Baada ya kuondoka bi Harisa akamfuata Kapona na kumwambia “nilijua mzee kajua juu ya mpango wetu” Kapona akajibu hatamimi nilijua ni hivyo hivyo.Ilipotimia miezi miwili bi Harisa akawa na kila dalili ya mimba.Ilikuwa usiku mida ya saa mbili,walikuwa mezani, yeye na mumewe,wakila chakula,mala bi Harisa akatoka mezani na kwenda kutapika.Mala mumewe akamuuliza “unaumwa tumbo?” bi Harisa akajibu hapana mimi siumwi ila najisikia kichefu chefu tu.Siku zikapita bi Harisa akaamua kumwambia mumewe:
Bi Harisa: mume wangu ninajambo jema nataka kukwambia.
Mzee Shabibu: jambo gani hilo mke wangu?
Bi Harisa: nimda mrefu tulikuwa tunalalamika kuhusu mtoto.Mungu
kasikia kilio chetu na hivi sasa nina mimba.
Mzee Shabibu: Ni kweli uyasemayo?
Bi Harisa: Ni kweli mume wangu, na nina uakika kwakile nikisemacho.
Raisi Shabibu akamwambia mkewe nimekuandalia sherehe nzuri ya kukupongeza mkewangu kwa kubeba mimba.Siku iliyofuata raisi akawaita watumishi wake wote na kuwaambia. “Leo ni siku ya kufanya usafi kwani kuna sherehe niliyo muandalia mkewangu kwakuwa amebeba mimba” kapona aliposikia akashtuka, alijua fika kuwa ile nimimba ya kwake.Mara raisi akamalizia kwa kusema, wote kafanyeni kazi isipokuwa Kapona aje.Kapona akaenda kwa wasi wasi, zaidi alipofika raisi akamwambia.
Raisi: Kapona naomba uniambie ukweli, nilipo ondoka hakuwahi kuja mwanaume yeyote humu ndani? Au mke wangu kutoka?
Kapona: Heshima yako raisi hakuwahi kutoka wala kuingia mtu yeyote humu ndani.
Raisi: Unasema ukweli wewe mkuu wa jeshi langu?
Kapona: Ninayo yaongea niyakweli mzee.
Raisi: Nakushukuru kwa ulinzi wako.
Kapona: Ahsante sana.
Baada ya Kapona kuongea na raisi, Kapona akaondoka.Ilipofika usiku Kapona alikuwa anawaza ndani ya kijumba chake.Mara akasikia hodi! Kumbe alikuwa ni mke wa raisi (bi Harisa).
Bi Harisa: Hodi! Hodi!
Kapona: Karibu, kwani wewe ni nani? “Aliuliza Kapona”
Bi Harisa: Ni mimi mpenzi wako.
Kapona: Ahaa! Zuhura tena karibu.
Kapona alijua ni Zuhura kwakuwa Zuhura ndio mpenzi wake na muda si mrefu wangefunga ndoa.Lakini haikuwezekana kwa sababu alimpa mimba hivyo akaahilisha ndoa yake.Mpaka muda huo Zuhura alikuwa na mimba ya miezi mitatu (3), wakati bi Harisa kipindi hicho alikuwa na mimba ya miezi miwili (2). Basi Kapona akafungua mlango, alipofungua akamuona mke wa raisi.Kapona akasema, karibu mke wa raisi.
Bi Harisa: Ahsante Kapona
Kapona: Karibu kiti bibie.
Bi Harisa: Wala sikai kwani sijamuaga raisi ila nilitaka kukwambia kitu.
Kapona: Kitu gani tenaa.Kama kufanya na wewe siwezi tena.
Bi Harisa: Hapana! Lakini:
Kapona: Lakini nini! (Kapona anamshangaa bi Harisa anavyo waza)
Bi Harisa: Hii mimba niliyokuwa nayo niya kwako.
Kapona: Sasa tufanyeje? Na je? mzee akijua itakuwaje?
Bi Harisa: Yeye anajua mimba hii ndio ya kwake.Na wala hatokuja kujua hata siku moja.
Kapona: Sawa! Lakini na mimi nataka kuoa baada ya Zuhura kujifunga.
Bi Harisa: Kapona mimi nakupenda je ukioa itakuwaje.
Kapona: Wewe umeolewa, lazima na mimi nioe, niruhusu tu nioe.
Bi Harisa: Sawa Oa lakini na kupenda sana.NDOA NJEMA.
Baada ya kuondoka bi Harisa, Kapona aliendelea kulala.Siku ya sherehe ikafika.Mzee Shabibu alikuwa na furaha sana akaanza kwa kusema. “Karibuni sana katika sherehe ya mke wangu kubeba mimba” walikuwa niwageni wenye hela zao matajiri kwa matajiri.Baada ya hapo watu walikula na kunywa, ilipofika jioni watu wakaondoka.Hatimaye mke wa Kapona aitwaye Zuhura akawa amejifungua mtoto wa kime akamwita NASRI.
Hatimaye miezi tisa ikafika, ilikuwa ni usiku wa tarehe 17 kuamkia tarehe 18,bi Harisa akajawa na uchungu,mumewake alipoona hali inazidi kuwa mbaya, akaamua kumchukua na kumpeleka hospital,hakukaa sana bi Harisa akawa amejifungua mtoto wa kike.Alikuwa ni mtoto mzuri lakini cha kushangaza hakufanana na baba yake yaani Kapona. Bali alifanana na mama yake bi Harisa.
Waandishi wa habari mbali mbali walikuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumpiga picha mtoto wa raisi wao.Kweli ni mambo yaliyo nyuma ya panzia,ndio maana wahenga wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza.Raisi alifurahi sana akajua kweli amepata mtoto,hakujua mtu yeyote Yule kwa ukweli ule zaidi ya bi Harisa na Kapona.Safari ya kurudi kwao wakitokea hospital ikaanza. “Huo ndio ukweli wa mke wa raisi”
Mtoto wa raisi aliitwa NUSRAT.Wakati mtoto wa Kapona anaitwa NASRI.watoto waliendelea kukua, baada ya miaka mitano, mtoto wa raisi akapelekwa shule akasome, Raisi akaamua kuamisha makazi yake mkoa jirani, wakati anaangaika na kuama.Bi Harisa akasema, “naitaji kuonana na Kapona,pamoja na mtumishi mmoja” akaenda kumwita Kapona.Alikuwa yupo ndani na mkewe,Yule mtumishi akagonga hodi na kusema.Samahani Kapona unaitw\a haraka sana na mke wa raisi.Kapona kusikia hivyo akashtuka na kusema kuna nini? Yule mtumishi akajibu “Sijui bari wakaongozana hadi kwa mke wa raisi.Alimkuta umesimama mlangoni anataka kuondoka.Wakati huo mtoto wake alikuwa ndani ya gari na baba yake wa kusingiziwa ( raisi ).Mke wa raisi alipo muona Kapona alifurahi sana akawa anatabasamu na kumwambia Kapona.
Bi Harisa: Najua unajua ukweli kuhusu hawa watoto, nakuomba endelea
kuchunga siri hii.
Kapona: Usijari nitaitunza.
Bi Harisa: Nakupa zawadi hii na uitunze sana, akafungua pochi na kutoa lundo la hela pamoja na kipande cha dhahabu.
Kapona: Ahsante sana, nakutakia safari njema wewe na mtoto wangu.
Baada ya maongezi hayo waliondoka, na Kapona akabaki akiwa sindikiza kwa macho.Alitamani aseme ukweli kwa sababu mtoto alikuwa mzuri sana.Raisi aliongozwa na msafara mkubwa sana wa magari.Ilipotimia saa kumi na moja jioni,walikuwa wamewasiri nyumbani.Ilikua nyumba kubwa na nzuri sana.Walipofika kulikuwa na watu wengi sana.Raisi aliamua kutembea kwa gari kwakuwa alihitaji kuona baadhi ya miji iliyokuwa imechafuka kwa ukame.Kulifanyika sherehe kubwa sana ya kuwapokea.Huyu Kapona alikuwa tajiri mkubwa sana,baada ya kuachiwa fedha pamoja na dhahabu.Maisha yalikuwa mazuri sana kwa Kapona.
Baada ya mwaka mmoja bi Harisa akaanza kuumwa,aliugua sana.Kipindi hicho mtoto wao alipelekwa shule ya bweni.Bi Harisa alipo ona anazidi kuumwa akamwambia mumewe, “naomba ukamfuate mtoto kwani hari yangu si nzuri” baada ya kusema hivyo raisi akatoka hadi nje na kumtuma mtumishi aende shuleni na kumfuata mtoto(NUSRAT) akapewa gari na kuondoka.Alipofika shuleni akakutana na mwalimu mkuu na akakubali Nusrat aondoke.Njiani Nusrat alimuuliza Yule mtumishi,kunanini hadi umekuja kunifuata? Yule mtumishi akajibu “mzee kanituma nikufuate eti anahamu na wewe.”
Nusrat akamuuliza tena, mbona huwa anakujaga kunifuata yeye au anakujaga kuniona na kuondoka.Samahani naomba uniambie? Mi sijui chochote alijibu mtumishi.Vipi mama yangu yupo nyumbani? Aliuliza Nusrat.Yupo,alijibu mtimishi wa raisi.Basi wakaendelea na safari yao hadi walipofika.Alipiga honi na kuingia ndani,Mara Nusrat akaingia ndani na kupakuta patupu,akaita dada(msichana wao wa kazi) akaitika na Nusrat akamuuliza mama yangu yuko wapi? Dada akamjibu nenda ghorofa ya juu kabisa ndipo yupo.Alipoenda alimkuta mama yake akiwa amelala huku akiwa amekondeana.Akamuuliza kulikoni mama? Mama yake akajibu, niugonjwa tu mwanangu.
Nusrat akakumbuka kuwa hajamsalimia mama yake ndipo alipo msalimia kisha wakaendelea na maongezi yao. Raisi aliporudi alimkuta Nusrat akiwa amenyong’onyea na kumuuliza nini kimekusibu mwanangu mbona umekuwa hivyo? “ni hali ya mama ndiyo inanifanya niwe hivi” alijibu Nusrat mtoto wa raisi wa kusingiziwa.Raisi akamwambia mwanae,haya nimambo ya kawaida tu.Mungu atakusaidia mwanagu.
Asubuhi ilipotimia bi Harisa akamwita mwanae kwa sauti ya huruma.Nusrat mwanagu njoo.Baada ya kwenda akamwambia “leo nahisi ni siku yangu ya mwisho, nakutakia maisha mema, ila naomba kuwa makini, na soma sana. Na pia naomba nikwambie ukweli, nikwamba huyu baba yako sio Baba yako!, Baba yako ni…………..!!!, kabla hajamalizia sentensi yake umauti ukamfikia.Nusrat akawa analia kwa uchungu na kuita jina la mama yake!, mamaaa mbona unaniacha peke yangu,nitakaa na nani mimi? Alizidi kulia,mara baba yake akawa ameingia,alipo muuliza akajibu mama ametutoka.Wakawa wanalia kwa pamoja sauti zile zikawafikia hadi watumishi wake raisi.
Ndipo msiba ulipo zagaa nchi nzima.Msiba ulipomfikia Kapona akashtuka sana kipindi hicho alikuwa shuleni akimpeleka mwanae katika shule anayo soma Nusrati.Nibaada ya taarifa kumfikia mwalimu mkuu.Kapona alitamani kumwambia mwanae Nasri lakini roho ilidunda.Akaamua kukaa kimya.Hapo Nasri alikuwa kidato cha tatu na pia Nusrati nae alikuwa kidato hicho hicho.Baada ya bi Harisa kufa,msiba ulipoisha ndipo Nusrati akarudishwa shuleni.Alipofika alikuwa mpweke na mwenye mawazo kila dakika.Hana raha,analia kila mda,alikuwa anabembelezwa na marafiki zake. “Nusrati usilie wewe vumilia na usome sana, Mungu atakujaaria tu” hayo nimaneno kutoka kwa rafiki yake, aliye itwa Sabha.
Siku hiyo Nusrati alikuwa amekaa darasani peke yake.Mara Nasri akamfuata na kumwambia:
Nasri: Abari yako Nusrati
Nusrati: Nzuri nikusaidie nini?
Nasri: Hapana nakupa pole tu
Nusrati: Ahsante! Nimeisha poa.
Nasri: Samahani kama hautojari “naomba uwe rafiki yangu”
Nusrati: Samahani naomba utoke, kwani umekosa marafiki?
Nasri: Nimependa kuwa na wewe.
Nusrati akaondoka kwa dharau, huku akiwa amekasirika, alipofika bwenini wenzake wakamuuliza, unanini wewe? Nusrati hakujibu kitu.Siku zikapita Nusrati akawa mtu wa furaha muda wote, hali iliyo mfurahisha sana rafiki yake Sabha.Siku moja Sabha akamwambia “Nusrati unajua nafurahishwa sana na hari yako siku hizi, napenda muda wote uwe hivyo” Nusrati akajibu, nimambo ya kawaida tu hayo nimeisha zoea! Mara akapita Nasri Nusrati akamuangalia sana, mpaka Sabha akamshtukia “oya vipi? Mbona hivyo” Nusrati akajibu, Aah!!! Nimambo ya kawaida tuachane nayo.
Siku hiyo, ilikuwa nisiku ya michezo.Nusrati akaingia uwanjani kucheza mpira.Wakati mpira unaendelea muda wote Nusrati alikuwa anamuangalia Nasri.Sabha akasema “inaelekea unampenda sana yule kaka! Nusrati akajibu ndio nampenda sana ila nashindwa, nitaanzaje wakati nimekwisha mkatalia, Sabha akasema nikazi ndogo sana nitakusaidia,napenda nikuone ukiwa ni mtu wa furaha muda wote.Huo ulikuwa nimda wa mapumziko.Mara kengere ikagongwa,na wanafunzi wakarudi madarasani.Huko darasani Nusrati mawazo yote yalikuwa kwa Nasri Muda wa kutoka ukafika wanafunzi wote wakarudi mabwenini kwao.
Siku ya pili Sabha alikuwa amekaa darasani peke yake,wakati Nusrati alikuwa anafua,ilikuwa ni siku ya usafi juma pili.Nasri akaingia na kumwambia Sabha “afadhali nimekuona, nina shida na wewe” Sabha akasema ni shida gani hiyo best?.
Nasri: Kwanza rafiki yako yuko wapi?
Sabha: Nani! Nusrati?
Nasri: Ndio.
Sabha: Yupo kule chini anafua
Nasri: Poa! Sasa sikiliza!
Sabha: Mhhhh!!?
Nasri: Nataka kukutuma kwa rafiki yako.Unajua kuwa nampenda
Sana, nimemwambia lakini amenikatalia.
Sabha: Usijari nitaongea nae leo
Nasri: Chukuwa hii zawadi na umpelekee (anatoa bahasha kubwa na
kumpa Sabha ili ampelekee Nusrati kule alipo)
Sabha: Poa nitampa
Nasri aliondoka akiwa na matumaini ya kumpata Nusrati,mwanamke aliye utesa moyo wake.Sabha akatoka darasani na kuelekea bwenini alipo Nusrati,na kumkuta Nusrati akiwa amelala. Akamuamsha na kumwambia “chukua mzigo wako” Nusrati akamuuliza “umetoka kwa nani?” Sabha akajibu kutoka kwa mpenzi wako.Nusrati kusikia hivyo akafurahi na kusema nipe huo mzigo.
Sabha akatoa bahasha na kumkabidhi Nusrati.Mara wakati anafungua, mama yao mlezi wa shule, yaani (matron) akawa amemuita Nusrati!, Nusrati kusikia hivyo akaitika na kuchukua ule mzigo akawa ameuficha katikati ya madaftari yake. Akatoka na kumfuata mlezi wao wa shule.”Nimekuja mama”alisema Nusrati,yule mama akamwambia “nilitaka kujua kama upo ndani mwanagu.Nimekuletea zawadi leo,akawa amempa Nusrati Biskuti,Nusrati alicheka na kusema ahsante sana mama,kumbe unanipenda.Akaondoka kuelekea bwenini.Alipo ondoka, akaenda chumbani kwake na kuanza kufungua ule mzigo,akakuta ua,kadi na barua. Barua yenyewe ilikuwa inasomeka hivi:
Sabha akatoa bahasha na kumkabidhi Nusrati.Mara wakati anafungua, mama yao mlezi wa shule, yaani (matron) akawa amemuita Nusrati!, Nusrati kusikia hivyo akaitika na kuchukua ule mzigo akawa ameuficha katikati ya madaftari yake. Akatoka na kumfuata mlezi wao wa shule.”Nimekuja mama”alisema Nusrati,yule mama akamwambia “nilitaka kujua kama upo ndani mwanagu.Nimekuletea zawadi leo,akawa amempa Nusrati Biskuti,Nusrati alicheka na kusema ahsante sana mama,kumbe unanipenda.Akaondoka kuelekea bwenini.Alipo ondoka, akaenda chumbani kwake na kuanza kufungua ule mzigo,akakuta ua,kadi na barua. Barua yenyewe ilikuwa inasomeka hivi:
Nusrati
Natumai mzima wa afya na unaendelea poa na masomo, nafurahi sana kama upo hivyo.
Dhumuni la barua hii nikutaka kukwambia kuwa nakupenda sana.Nusrati,sijamuona mwanaume mzuri kama wewe, katika dunia hii.Pls naomba unikubarie ombi langu nipo radhi kwa chochote juu yako,nakupenda sana umeuteka moyo wangu,sijui umenipa nini make sili,sisomi,wala silali,yote hayo ni kwa ajiri yako mpenzi.Nikubalie unitoe katika jangwa la mawazo.Wako mpenzi.
Nasri
Nasri
ILOVE YOU.
Nusrati alifurahi kuona hiyo barua na akatokea kumpenda sana Nasri.Siku iliyofuata Nusrati akiwa darasani mara akamuona Nasri, alifurahi. Akaacha tabasamu pana, na Nasri akamjibu kwa kumrudishia tabasamu.Alipofika akamsalimia kisha akasema “jana ulipata mzigo wangu?”Nusrati akajibu ndio nimeupata ahsante sana.Nasri akamuuliza kwaiyo itakuwaje? Nusrati akajibu “hata mimi nakupenda sana,naomba unisamehe kwakuwa ile siku nilikutukana, usijari ni kawaida, alijibu Nasri huo ndio ukawa mwanzo wa mapenzi yao.Yakawa yanaanza na mapenzi yakazidi, walipendana kupita maelezo.Sabha alifurahi sana kila alipomuona Nusrati na Nasri alipenda sana kila wakati wawe ni watu wa furaha.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wawili hao waliopendana.Siku zikapita bila ya mtu kugundua zaidi ya rafiki yao Sabha.Kwa upande wa baba yake Nasri,yaani Kapona alipata kazi akawa mmoja wa wafanyakazi wa ofisi ya dhahabu Tanzania, kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha anahesabu mizigo yote inayo ingia na kutoka.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wawili hao waliopendana.Siku zikapita bila ya mtu kugundua zaidi ya rafiki yao Sabha.Kwa upande wa baba yake Nasri,yaani Kapona alipata kazi akawa mmoja wa wafanyakazi wa ofisi ya dhahabu Tanzania, kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha anahesabu mizigo yote inayo ingia na kutoka.
Alifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, hatimaye akaamua kufungua ofisi yake iliyoitwa.KAPONA GOLD COMPANY LIMITED.
Nayo ilikuwa inahusika na dhahabu, ilijulikana sana kampuni yake.
Siku moja akiwa kazini kwake mara akaingia polisi na siraha mkononi, walienda moja kwa moja hadi kwa msaidizi wake, na kumuuliza “bosi wako tumemkuta?” Yule msaidizi wake akajibu “yupo” huku akitetemeka polisi hao waliondoka moja kwa moja hadi ofisini.Walimkuta akiwa akifanya kazi zake na kumwamuru aache kila kitu na yupo chini ya ulinzi.Alishangaa na kuuliza “nini kosa langu?” akajibiwa utaenda kujua huko.Basi wakaondoka nakwenda hadi nje na kupanda karandinga na kuondoka.Walipo fika kituoni akakutana na mkuu wa polisi na wakaongea.Maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mkuu: Unajua kosa lako?
Kapona: Hapana!
Mkuu: Unahusika na wizi wa dhahabu ambazo waliiba katika ofisi
ambayo ulikuwa unafanya kazi zamani.
Kapona: Alishangaa na kusema “sihusiki na chochote mimi labda ni
mbinu zao tu.
Mkuu: Hapa hautoki mpaka kwa dhamana, je yupo mtu wa kukutolea dhamana? Na si kwa sasa, bali mpaka uchunguzi ufanyike sawa sawa.
Kapona: Sawa!
Mkuu: Kwa sasa unaweza kwenda ila utahitajika baada ya siku tatu.
Kapona: Sawa mkuu!
Uchunguzi ulifanywa kwa muda, na kugundua kuwa Kapona hakuwa na hatia.Hivyo aliitwa polisi na kupewa ruhusa ya kurudi nyumbani akiwa huru.Baada ya hapo Kapona aliondoka na kuelekea nyumbani kwake.Lakini alikuwa amekwisha msahau mwanae Nusrati, hivyo hata kama akimuona itakuwa ngumu kumkumbuka kama ndiye mtoto wake.
Nusrati alifurahia maisha na kumsahau mama yake ambaye ni marahaemu.Siku moja akiwa darasani mara akaingia madamu wao na kusema “Nusrati pamoja na Sabha na waomba.Nusrati pamoja na mwenzake Sabha walinyanyuka na kuondoka kumfuata madamu wao, huku Nasri akimuangalia sana Nusrati.Waliondoka moja kwa moja hadi ofisini kwa mwalimu mkuu na kumuona baba yake Nusrati.baada ya baba yake kumuona mwanae alifurahi sana.Waliongea na baba yake aka muachia hela nyingi za matumizi,muda huo alikuwa kidato cha tatu,na ilibaki wiki moja wafunge shule.Baba yake alikuja kumsalimia kwakuwa anatakiwa kwenda kikazi nchini Saudia Arabia.
Baba yake alimwambia mwanae “kuwa nimeoa mke mwingine ukija nyumbani utamuona, na nina omba umuheshimu kama mama yako mzazi.” Nusrati akajibu usijari baba, mimi nitamuheshimu kama mama yangu. Baada ya hapo raisi akaondoka na kumuacha Nusrati aendelee na masomo yake shuleni hapo.
Baada ya baba yake kuondoka Nusrati alimfuata Nasri na kumwambia “umemuona baba yangu leo?” Nasri akajibu hapana, sijamuona baba mkwe wangu.Wote walicheka na kuondoka kuelekea katika bustani kubwa iliyopo pale shuleni.Kwakuwa ulikuwa ni muda wa mapumziko, hivyo walikaa muda mrefu na kujadili maisha yao. “unajua Nusrati nakupenda sana hakuna msichana mwingine atakae nishauri eti nisimamishe penzi langu kwako” Nusrati akajibu “ata mimi nakupenda sana natamani siku moja tuwe mke na mume,wote wakacheka na kuendelea na maongezi yao.
Siku moja Nusrati alichukua daftari la Nasri ili asome kuna baadhi ya vitu alitaka kusoma.Mara kwenye kufunua akakutana na barua iliyokuwa inatoka kwa msichana mwingine aliye muandikia Nasri.Nusrati alikasilika sana.Hata Nasri alipokuja, aligundua kitu na kumuuliza.
Nusrati: “Una nini mpenzi wangu?” Nusrati akamjibu, hivi! unawapenzi wangapi?
Nasri: Kwani kuna nini mpenzi wangu?
Nusrati: Nijibu swali nililo kuuliza!
Nasri: Ni wewe tu mpenzi wangu!
Nusrati: Na huyu Gress ni nani yako?
Nasri: (Anacheka)
Nusrati: Kwaiyo mimi ni chizi au ndo unanidhalau?
Nasri: Si kama nakudhalau (huku akiwa anacheka)
Nusrati: Ila!, Hivi nikwambie mara ngapi? Nakupenda sana lakini. (kwa asira akaondoka)
Nasri: Nusrati! Nusrati!
Nusrati: Usiniite.
Nasri: Akainama chini huku akiwaza nijinsigani atamrudisha Nusrati, mara akatokea rafiki yake.Goerge na akamuuliza.
George: Vip mshikaji wangu mbona umekaa kimya?
Nasri: Bwana we acha tu, ni Nusrati huu ananisumbua.
George: Vipi amekasirika?
Nasri: Bwana kakuta sms ya Gress kwenye daftari langu.
George: Kwani ilikuwa inasemaje? Mpaka akasirike?
Nasri: Gress alikuwa ni mpenzi wangu kabla ya Nusrati sasa kunasiku alinitakia hali na nikasahau na kuiweka katika daftari zangu za summary.Sasa Nusrati leo kaiona hapo ndio kosa.
George: Inabidi ukamuombe msamaha, au umwambie ukweli.
Nasri: Poa nita mwambia.
Siku ilyofuata Nasri alikuwa amekaa darasani.Mara akamuona mtu kwa nje akiwa chini ya mti,alipo muangalia kwa umakini aligundua kuwa ni Nusrati.Alimfuata, na alipo mkalibia alimkuta Nusrati akiwa analia kilio cha kwikwi.Alimuita jina lake “Nusrati” Nusrati alipogeuka alikutana na mpenzi wake Nasri.Nusrati akazidi kulia.Hapo Nasri ndipo akasema “Naomba unisamehe sana mpenziwangu” Nusrati akujibu chochote kile.
Nasri: Nusrati jua kuwa nakupenda sana na sipo tayari kukuacha.Tafadhali naomba unisamehe.
Nusrati: Hauna mapenzi ya kweli kwangu, kama unanipenda kwa nini una msichana mwingine? Hapo ndipo Nasri aliamua kumwambia Nusrati ukweli na akumficha kitu chochote.Nusrati alikaa kimya na kusikiliza muda wote.
Nusrati: Mbona hukuniambia mapema mpenzi wangu?
Nasri: Samahani nilijua utaniona mimi labda ni Malaya.
Nusrati: Usijari nimekusamehe.wewe ni mume wangu wa ndoa.
Hapo wakakumbatiana na kuondoka wote hadi darasani.Wakakutana na George njiani.George alipo waona alicheka sana.Nusrati akamuuliza “mbona unacheka George?” George akajibu hapana nimefurahi tu.Nusrati “poa kama ni kweli”, George akamuuliza Nasri, vipi mshikaji wangu umefanikisha! “Nimefanikisha broo” alijibu Nasri.George akasema poa.Wakaendelea na safari yao.
Siku ya kufunga shule ikafika.Wazazi walipigiwa simu na walimu ili waje kuwachukuwa watoto wao.Ilipofika saa 4:30 asubuhi, mtumishi wa raisi aliwasili shuleni ili kumchukua mtoto wa raisi Nusrati.Nusrati alipoliona gari lao, akaanza kumtafuta Nasri.Alipo muona akamkumbatia na kumwambia “likizo njema mpenzi wangu” Nasri akajibu “nawe pia kuwa makini sana” usijari alijibu Nusrati.
Baada ya hapo Nusrati alipanda kwenye gari na kuondoka zake.Huku Nasri akimsindikiza kwa macho.
Siku ya kufunga shule ikafika.Wazazi walipigiwa simu na walimu ili waje kuwachukuwa watoto wao.Ilipofika saa 4:30 asubuhi, mtumishi wa raisi aliwasili shuleni ili kumchukua mtoto wa raisi Nusrati.Nusrati alipoliona gari lao, akaanza kumtafuta Nasri.Alipo muona akamkumbatia na kumwambia “likizo njema mpenzi wangu” Nasri akajibu “nawe pia kuwa makini sana” usijari alijibu Nusrati.
Baada ya hapo Nusrati alipanda kwenye gari na kuondoka zake.Huku Nasri akimsindikiza kwa macho.
Mara baada ya kuondoka Nusrati, gari likaja na Nasri alipoangalia kwa umakini alikuta kuwa ni gari la baba yake,naye akaondoka kuelekea bwenini na kuchukua vifaa vyake na kuongoza hadi ofisini na kusalimiana na baba yake na kuondoka.Wakati rafiki yao Sabha alikuwa wa kwanza kuondoka.
Baada ya muda Nusrati alifika kwao.Na kweli alipokwenda alimkuta mama mpya, mama huyo alijulikana kama bi Habiba. Bi Habiba alipomuona Nusrati alifurahi sana.
Bi Habiba: Karibu sana mwanangu
Nusrati: Ahsante Sana mama
Bi Habiba: Habali ya shule mwanangu
Nusrati: Nzuri tu mama, nimefurahi Sana kukuona kwani baba alipokuja shule aliniambia kuwa ameoa nikajawa na hamu ya kukuona.
Bi Habiba: Hata Mimi nilimwambia baba yako tuje wote lakini alikataa.
Nusrati: Hakuna mbaya mama.Ila nimechoka Sana.
Bi Habiba: Pole mwanangu, kabadili nguo na uoge kisha uje ule. Kweli
Nimekuandalia chakula kizuri sana mwanangu.
Nusrati: Ahsante mama yangu.
Baada ya kuoga na kubadili nguo.Nusrati alijilaza kitandani na kufungua simu yake na kumtafuta Nasri. Lakini Nasri muda huo alikuwa hapatikani..Nusrati akatoka na kwenda kula,huku akiongea na mama yake.Alipoludi chumbani alikuta ‘’missed call’’ ya mpenzi wake Nasri.Hapo akampigia na kuongea nae:
Nusrati: Haloo!
Nasri: Ohoo my dear! Vipi ulifika salama?
Nusrati: Nimefika salama tu vipi wewe?
Nasri: Hata mimi baba alikuja kunichukua baada ya muda tu, ila nimefika salama mpenzi wangu.
Waliendelea na maongezi yao.Baada ya wiki moja raisi alirudi, alipofika nyumbani kwake alifurahi kumuona mkewe akiishi vizuri na mwanae.
Siku moja Nusrati alimuomba ruhusa baba yake anataka kwenda kwa rafiki yake.Kwakuwa raisi alimpenda sana mtoto wake alimruhusu.Nusrati alijiandaa kisha akatoka nje na kuchukua moja ya gari na kuondoka kuelekea kwa akina Nasri.Akuitajika msimamizi,alipokuwa kwenye gari alimpigia Nasri na kumwambia kuwa anakuja.Nasri alifurahi sana,akamwambia mama yake na kuandaa chakula kizuri. Baba yake Nasri alikuwa amesafiri.
Basi baada ya muda Nusrati akapiga honi katika nyumba ya akina Nasri, mlinzi akafungua geti ndipo Nasri alipotoka na kumkumbatia Nusrati,wakaongozana hadi ndani.Walipofika wakamkuta mama yake Nasri amekaa kwenye kochi.Nusrati alimsalimia mama yake Nasri.Nusrati alikaa kwa muda pale nyumbani kwa akina Nasri, kisha akaondoka.Wakati Nusrati anaondoka alimuuliza Nasri “mbona baba sijamuona?” baba amesafiri alijibu Nasri.Basi akapanda gari na kuondoka kuelekea nyumbani kwao alifurahi sana.
Likizo ikaisha Nusrati akarudi shule,alipelekwa na mama yake wa kambo.Alipofika shuleni alimkuta Nasri amekwisha fika,wakaendelea na masomo kama kawaida.Hatiye mwaka ukaisha wakamaliza kidato cha nne na kuwa watoto wa uraiani.Baada ya miezi mitatu matokeo yakatoka,wote walikuwa wamefauru mitihani yao na kuweza kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.
******************************************************
Baada ya miaka mitano wote walikuwa wamemaliza masomo yao.Waliporudi nyumbani kwao kila mmoja alikuwa na ndoto zake.
Siku hiyo mzee Shabibu alimuita mwanae na kumwambia.
Mzee Shabibu: Mwanagu najua kuwa umemaliza masomo na umeisha kuwa, sasa ni wakati wako wa kujipanga.
Nusrati: Nikweli baba, na sasa nahitaji kufanya kazi nipo katika mikakati ya kutafuta.
Mzee Shabibu: Usijari mwanangu mimi baba yako nipo utapata kazi.Je nikazi gani unataka? Ila, nitakupa nyumba pamoja na kampuni yangu uwendeleze pamoja na kuvitunza kama mimi nilivyo kuwa navitunza.
Nusrati: Nitafurahi sana, na ahsante sana baba yangu.
Baada ya kuonge na baba yake, alimtafuta Nasri kwenye simu yake na kumwambia yote yaliyojili nyumbani kwao.Nasri naye akasema “hata mimi baba ameniajiri kwenye kampuni yake kama muhasibu mkuu” ooh! Ongela sana mpenzi wangu, maisha yetu yatakuwa ni mazuri sana alisema Nusrati.
Baada ya watu hao kuanza kazi.Siku moja Nasri alimpigia simu Nusrati na kumwambia
Baada ya watu hao kuanza kazi.Siku moja Nasri alimpigia simu Nusrati na kumwambia
Nasri: Vipi dear umeishatoka kazini?
Nusrati: Bado kunakazi naimalizia ila muda si mrefu nitaondika.
Nasri: Sawa,ila naomba ukitoka pitia nyumbani. Mimi niponjiani na elekea nyumbani.
Nusrati: Sawa mpenzi wangu.
Baada ya muda kama nusu saa Nusrati alitoka kazini na kwenda moja kwa moja hadi kwenye maegesho ya magari na kuchukua gari lake, mara akatokea mmoja wa wafanyakazi na kumwita.Bosi!,mara Nusrati akasimama.Alipomkalibia bosi wake akasema “samahani bosi kuna baadhi ya mikataba imeletwa sasa hivi.Nusrati akajibu “kaniwekee ofisini kesho nitaisaini au niya haraka?” hapana,alijibu yule mfanya kazi.
Nusrati aliendelea na safari yake.Baada ya muda akawa amefika nyumbani kwa akina Nasri akapiga honi na mlinzi akafungua geti.Akashuka na kuongoza moja kwa moja hadi ndani,Nusrati alipofungua mlango alimkuta Nasri akiwa amekaa sebleni, Nusrati akamkumbatia na kumsalimia.Wakaanza maongezi yao:
Nasri: Unajua nimekuita hapa ili tuongee zaidi kuhusu maisha yetu mpenzi wangu.
Nusrati: Sawa na nivizuri sana.
Nasri: Sasa tumekaa muda mrefu, inabidi tuweke wazi penzi letu na hata ikiwezekana tufunge ndoa.
Nusrati: Sawa mume wangu.
Nasri: Usijari, ni muda mfupo umebaki utaniita mume wangu, hasa baba watoto.
Nusrati: Sawa.
Baada ya muda Nusrati alimuaga mpenzi wake na kuondoka zake.Alipofika alioga na kulala,akiwa kitandani alimpigia simu mama yake bi Habiba na kumwambia “mama yangu kuna kitu kizuri sana nataka kukwambia kesho nitakuja” bi Habiba alifurahi sana,akasubiri siku inayofuata.Kipindi hicho Nusrati alikuwa hakai nyumbani kwao.Tayari alikuwa anakaa katika nyumba aliyopewa na baba yake mzee Shabibu.
Siku ya pili Nusrati alitoka nyumbani kwake asubuhi na mapema, aliondoka na kwenda moja kwa moja hadi kwa mama yake wa kambo bi Habiba.Alimkuta bi Habiba anakunywa chai, alimsalimia, na bi Habiba aliitikia kwa furaha sana.Na baada ya hapo bi Habiba akasema:
Bi habiba: Karibu mwanagu.
Nusrati: Ahsante mama yangu.
Bi habiba: Nakuona unafuraha sana leo, kwani unanini?
Nusrati: Nikweli mama, leo nina furaha sana kwani kunajambo nataka kukwambia.
Bi habiba: Jambo gani hilo mwanangu?
Nusrati: Mama unajua kuwa sasa tayari nimekuwa, nina kazi pamoja na nyumba yangu.Sasa mama nimepata mchumba nataka kuolewa mama.
Bi habiba: Vizuri sana mwanagu, napia nakupongeza kwa kujichunga muda wote, napia nakuhaidi kuwa nitasimamia ndoa yako kama mama yako. Na ninaomba unioneshe huyo mwanaume.
Nusrati: Sawa mama nitamleta.
Bi habiba: Ila nitakwambia siku ya kumleta, mpaka nimwambie baba yako kwa kuwa anakupenda nahisi atafurahi sana kusikia hivyo.
Nusrati: Sawa mama, ngoja niondoke niende kazini.Ila usisahau mama.
Bi habiba: Wala sitasahau mwanagu.
Baada ya Nusrati kuondoka, mama yake aliendelea na kazi zake kama kawaida.
Nusrati alipofika kazini alimpigia simu Nasri na kimwambia yote ambayo ameongea na mama yake.Nasri alifurahi sana kwa uamuzi aliofanya Nusrati.Nakumwambia kuwa nayeye ataenda kuongea na wazazi wake.Nusrati alifanya kazi yake na muda ulipofika aliondika kuelekea nyumbani kwake.
Akiwa nyumbani kwake anakula mara simu yake ikaita, kuangalia ni mama yake.Alipokea na kumsalimia “shkamoo mama” alisema nusrati.
Akiwa nyumbani kwake anakula mara simu yake ikaita, kuangalia ni mama yake.Alipokea na kumsalimia “shkamoo mama” alisema nusrati.
Mama yake akasema “Nusrati mwanangu, baba yako anakuitaji.kesho asubuhi uje” sawa mama nitakuja, alijibu Nusrati.
Asubuhi ilipofika Nusrati aliondoka mpaka nyumbani kwao, ilikuwa ni siku ya mapumziko (juma mosi).Alipofika alimkuta baba na mama wamekaa tu.Akawasalimia shkamooni wazazi wangu, kwa pamoja wakaitikia marahaba mwanetu. Baada ya salamu Nusrati akaanza kuongea na baba yake.
Mzee Shabibu: Mwanangu nimepata habali zako kutoka kwa mama yako, sasa nitakuandalia sherehe ya kumtambilisha mchumba wako.
Nusrati: Sawa baba!
Mzee Shabibu: Ila huyo mwanume anaitwa nani na anafanya kazi gani?
Nusrati: Anafanya kazi katika kampuni ya Kapona.KAPONA GOLD CAMPANY LIMITED.
Mzee Shabibu: Vizuri sana kwa kuchagua mume anayefanya kazi kama wewe mwanangu.
Nusrati: Ahsante
Baada ya maongezi hayo Nusrati alimpigia simu Nasri na kumwambia habari zote, Nasri alifurahi sana.Nasri naye akamwambia mama yake, kwa kuwa baba yake alikuwa amesafiri na alikuwa bado ajarudi kutoka safari
Ilipofika usiku Nasri alimpigia simu baba yake na kumwambia hivi:
Nasri: Shkamoo baba
Baba Nasri: Marahaba mwanangu
Nasri: Habari za siku
Baba Nasri: Salama za hapo nyumbani?
Nasri: Nzuri tu baba.Baba nina habari njema nataka kukwambia.
Baba Nasri: Habari gani?
Nasri: Baba unajua kuwa sasa tayari nimekuwa, naisitoshe nimepata mchumba.
Baba Nasri: Vizuri sana mwanangu.
Nasri: Naistoshe juma mosi naenda kutambulishwa kwao.
Baba Nasri: Sawa mimi nitakuwa nina kazi, ila mama yako atakwenda.Mimi nitakuja siku yandoa mwanangu sawa.
Nasri: Sawa baba.
Nasri: Sawa baba.
****************************************************
Siku ya juma mosi ikatimia, kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wame alikwa na raisi.Basi bwana! Ikawa kama siku ya harusi,kumbe ilikuwa ni siku ya utambulisho tu.Nusrati alipendeza sana pembeni alikuwa na Nasri.Nusrati alisimama na kumlisha keki mtu mmoja mmoja kwa upande wa Nasri.Wakati ulipofika raisi akasema, napanga kabisa siku ya ndoa,alipomaliza kusema,watu waliondoka ila mama Nasri alibaki ili wazungumze na wazazi wa Nusrati.Walipomaliza kuongea,mama Nasri akaondoka.
Hatimaye siku ya ndoa ikafika, nibaada ya miezi miwili tu.Tangu Nasri atambulishwe.Wakiwa ndani ya gari, Nasri pamoja na mshenga wake, Nasri alisema “siamini kama leo namuoa Nusrati.” Usijali ila kilichobaki ni uaminifu tu, alisema mshenga.
Wakati wa zoezi la ufungishaji ndoa linaendelea.Kabla ya ndoa haijafungwa, mara ikasikika sauti iksema. No! No! No! THIS IS MY BLOOD.Nusrati is my beby, watu wote waligeuka na kumtazama yule mtu.Nasri aligundua kuwa ni baba yake.Lakini hakujua kwanini alisema hivyo.Habari zilimfikia Nusrati ndani, aliposikia alishtuka sana.Kapona akaendelea kusema hivyo hivyo.Raisi aliomba zoezi lisitishwe, na kumtafuta yule mtu na kukaa nayechini na kuanza kuongea.
Raisi: Haa! Kapona siamini kama watoto wetu wanafunga ndoa
Kapona: Hapana raisi kwanza naomba unisamehe sana.Kwakitendo nilichofanya.Kapona aliadithia hadithi yote yaani ukweli uliopo baina ya Nasri na Nusrati.
Raisi: No! Kapona unanitania.Kwanini ulitembea na mke wangu, lazima nikuuwe.
Kapona: Hapana usiniuwe.
Raisi alikasirika sana.Lakini bi Habiba alimpunguza hasira na akawa hana tena ujanja,akaamua kukubali ukweli.Kimbembe kilikuwa kwa Nusrati,alilia sana kila walipo mbembeleza alikataa mwishowe akasema.Lazima nijiuwe kwa sababu siwezi kutembea na kaka yangu.Nusrati alikimbia hadi kwenye ghorofa la juu nia yake ajiuwe.Alipofika kule juu anataka kujiuwa anaangalia chini akamuona baba yake pamoja na raisi wana muulizia hapo hapo,Nusrati akadondoka kwa nyuma na kuzimia.
Watu walimuokota na kumpeleka hospital.Nasri alilia sana.Hakuwa na jinsi,aliupokea ukweli kuwa yule ni dada yake baba mmoja.Baada ya siku mbili waliitwa na raisi na kuanza kuwaambia kuwa.Naombeni mmsamehe marehemu mke wangu kwa uovu aliofanya. Napia kuweni makini sana.Nawatakia maisha mema.
Watu walimuokota na kumpeleka hospital.Nasri alilia sana.Hakuwa na jinsi,aliupokea ukweli kuwa yule ni dada yake baba mmoja.Baada ya siku mbili waliitwa na raisi na kuanza kuwaambia kuwa.Naombeni mmsamehe marehemu mke wangu kwa uovu aliofanya. Napia kuweni makini sana.Nawatakia maisha mema.
Nusrati alilia huku akisema, mama! mama! Kwanini ukuniambia mapema? Mpaka haya yote yanatokea.
Mzee Shabibu( raisi ),alisema usimlaumu mama yako, ila muombee mema huko alipo.Nawatakia maisha mema.Baada ya hayo Nasri na Nusrati wakaombana msamaha na kuendelea na maisha, japo Nusrati alikuwa mtoto wa Kapina,ila raisi alimjari kama zamani. Huo ukawa mwisho wa mapenzi yao na ukawa mwanzo wa maisha ya kaka na dada.