Utafiti waonesha Mwigulu Nchemba atashinda Urais 2015. Wanafunzi wa vyuo vikuu, Walimu, Wafugaji, Wafanyakazi, Watoto wa masikini , Wanyonge, Wakulima, watanzania waishio nje ya nchi na vijana wa vijiweni waapa kutembea kwa miguu na kumchangia ashinde kwani ndiye mtetezi wa wanyonge. Wananchi wa Iramba wampa Baraka zote.
Mwigulu Nchemba alimaarufu SOKOINE WA PILI & MTETEZI WA WANYONGE Akiwa bado hajatangaza nia yake rasmi ya kugombeaUrais 2015, utafiti wa moja ya taasisi (Jina limehifadhiwa kwa usalama) unaonesha kuwa mzalendo huyo anazaidi ya asilimia 75 ya kushinda Urais ndani ya chama na ndani ya umma kutokana na msimamo wake wa kutetea wanyonge kwa kufa na kupona.
Kwa upande wa vyuo vikuu wamesema huyo ni mtetezi wao tangu angali mbunge wa kawaida alipeleka hoja binfsi ya watoto wa masikini kuwa na mfuko wa kuwakopesha asilimia mia moja punde akipata chuo. Mwigulu amekuwa akisisitiza bungeni kuwa mtoto wa masikini aliyesoma shule za kata kwa wazazi au walezi wake kuuza vitumbua na kufaulu, na kwenda kidato cha sita kwa wazazi au walezi wake kuuza matembele akafaulu, anapopata chuo na kukosa masomo ni kuangamia kwa maisha yake na familia yake nikuendelea kuwa masikini zaidi.
Mwigulu anayajua haya kwakuwa yeye mwenyewe anatokana na watu masikini na ameishi na kukua akiwa na watu masikini. Wanafunzi wa vyuo vya juu na waliokosa mikopo na walioko sekondari wanaombea chama chake kimteue Mwigulu aliyemtetezi wao, anayeguswa na maisha yao ili watoto wa masikini wapate mikopo. Mara zote Mwigulu amekuwa akisisitiza kubana matumizi ili fedha zikasomeshe watoto wa masikini, katika bunge la bajeti Mwigulu alisema misamaha ya kodi kwa matajiri ifutwe ili fedha ile ikasomeshe watoto wa masikini, wakwepa kodi wabanwe ili fedha hizo wakopeshwe watoto wa masikini, hata bunge la katiba Mwigulu alisema kama theluthi mbili haina uhakika na hakuna maridhiano bunge lifutwe na fedha hiyo ikopeshwe kwa wanafunzi zaidi ya 40,000 waliokosa mikopo. Na hivi majuzi Mwigulu amesema fedha zilizookolewa bungeni na zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kura ya maoni wakopeshwe watoto wa masikini wote waliokosa mikopo huku wakiwa na sifa na nafasi ya kujiunga vyuo vikuu.
Zipo tetezi kuwa viongozi wa bunge maalumu wamemwomba rais akubali wagawane kila moja milioni ishirini kwa kila mjumbe wote wa bunge maalum. Hivi majuzi maraisi wote wa serikali za wanafunzi walisema mtu anayefaa kuongoza Taifa hili ni Mwigulu kwa sifa zifuatazo, Ujasiri, uzalendo, uadilifu, uchapakazi, kujali wa nyonge, vision yake ni nzuri kuhusu maendeleo, vision yake ni nzuri kuhusu rasilimali ya Tanzania kuwanufaisha watu wote hasa masikini, uwazi, ukweli, utaalam uliobobea wa uchumi, uhodari wa kukemea wezi bila uoga tena akiwa Rais akubali atumie jina la "SOKOINE WA PILI". Sisi wanavyuo tutazungusha form yake na tutapiga kampen vijijin kwa gharama zetu.
Kwa upande wa walimu na wafanyakazi wanaomba Mwigulu ateuliwe na chama chake iliwamvushe kwenye kura ya jumla na awe Rais kwani amekuwa mtu pekee anayejali masilahi yao. Mwigulu alianzisha vita na wafanyabishara matajiri bila kuhofia maisha yake akiwataka walipe kodi ili kuwapunguzia mzigo wa kodi wafanyakazi wao wasioweza kukwepa kodi na kuwaongezea mishahara. Mwigulu alisema hatuwezi kusamehe kodi matajiri, tukaacha matajiri wakwepe kodi halafu tukawakamua na kuwanyonya wafanyakazi kwa kodi kubwa, mishahara kidogo na kusababisha wapigike na maisha magumu.
Hivi majuzi mwigulu alianzisha vita ya mishahara hewa kitu kilichowa wafanya walimu na wafanyakazi waone Mwigulu ni mkombozi wao kwani wamekuwa wakiishi maisha magumu huku watu wengine wakipokea fedha bila kufanya kazi, Mwigulu ameokoa zaidi ya bilioni 40, kila mwezi zilizokuwa zinakwenda kwenye mishahara hewa. Walimu wamesema madai yao yamekuwa yakikwama serikali huku kwa uzembe serikali ikilipa watu hewa, Mwigulu amekuwa tumaini jipya kwa walimu, zipo taarifa kuwa Mwigulu alipoambiwa mahitaji ya walimu yakiwepo ya Muundo wa utumishi na Chombo cha ajira cha walimu aliyapigania kwenye chama na serikali hadi yakakubaliwa, ndio maana NKM wa walimu ndugu EZEKIEL OLUOCH alisema waziwazi bungeni kuwa Mwigulu Nchemba anafaa kuwa Rais na anawaomba watanzania wamfikirie kumpa nafasi hiyo.
Kwa upande wa wafugaji, wanatambua Mwigulu ni mtoto wa mfugaji ambaye amekuwa akisimama imara kutetea maslahi ya wafugaji, itakumbukwa Mwigulu kwenda Loliondo na kuwarudishia wafugaji eneo lao la kufugia walilokuwa wamepokwa. Mafugaji pia wanampenda Mwigulu kwa ujasiri wake ikiwa ndio sifa kuu ya jamii ya kifugaji, ikumbukwe watu wa Loliondo ndio waliombatiza Mwigulu kuwa ni "SOKOINE INGINE".
Kwa upande wa watoto wa masikini , wanyonge na vijana wasio na ajira wamepata matumaini na Mwigulu kwa ajili ya ujasiri wake wa kusimamia maslahi ya wanyonge,. Mwigulu amekuwa akisimamia kodi ipatikane ikatumiwe kuwaendeleza wanyonge, Mwigulu amekuwa akitaka vijana wapewe ajira badala ya kuhamisha watu waliofuja pesa eneo lingine, pia amekuwa akisisitiza watu wasikaimu nafasi nyingi ilihali vijana hawana ajira. Na hivi majuzi Mwigulu alisema tunalipaje watu hewa wakati vijana wapo mtaani hawana ajira na hawajaajiriwa kwa kigezo cha ufinyu wa bajeti.
Taarifa za ndani ya chama zinaonesha kuwa Mwigulu Nchemba ndiye Mwanasiasa mwenye mvuto na mwenye kukubalika zaidi ndani ya chama kwa kutumia vigezo vya hoja, maadili, uwezo wa uongozi, utu, uzalendo, mabadiliko kwa vitendo, akimfuatia Rais Kikwete kwa wengine wanakubalika kwa mbinu hivyo kikosi kazi cha utafiti kiliona Mwigulu atashinda Urais kwa urahisi. Taasisi iliuliza watu milioni 2.8 kwa njia tofauti ikiwepo mitandao ya kijamii majibu ilikuwa CCM IKITAKA KUSHINDA KIRAHISI URAIS 2015 IMTEUE MWIGULU NCHEMBA kwani anakubalika na wanyonge na anatumainiwa na wanyonge kwani ndio MTETEZI WA WANYONGE.
UPANDE WA WANANCHI WA JIMBO LA IRAMBA, WANANCHI WA IRAMBA WAMEMPA BARAKA ZOTE AGOMBEE URAIS, NA WAMEJIRIDHISHA KUWA ANATOSHA KWA NAFASI HIYO. Kwa nyakati tofauti timu ya utafiti ilipita kata kumi na sita kati ya kumi na saba, majibu yalikuwa Mwigulu akirudi jimboni tutampitisha bila kupingwa, NI RAIS wetu sisi, lakini tumesikia anatakiwa kitaifa, anabaraka zetu zote, sisi ni mashahidi, huyu ni kiongozi, anasifa za kutukuka. Anatosha. Tunahitaji mabadiliko kwa vitendo.
Kwa upande wa kata moja ambao hawakutaka awe Rais walisema bado wanamhitaji jimboni kwani hawajawahi kupata mbunge kama huyu, hawajawahi kuwa na kiongozi bora kama huyu hivyo aachwe wamfaidifaidi.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo.