Siku ya jana ilisikika miripuko minne mikubwa uko eneo la Mbagara rangi tatu nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Jambo ambalo liliwashtua wakazi wengi wa eneo hilo, uku baadhi ya akina mama wakikimbia na watoto wao migongoni wakihofia kuwa yaweza kuwa ni moja ya miripuko ya mabomu.
Kwa mujibu wa msimuliaji wa tukio hili, amesema kwamba miripuko hiyo ilisikika kuanzia mida ya saa 11:35 asubuhi, kisha ikazimika gh'afra.
Mbali na kusikika kwa miripuko hiyo bado chanzo chake hakijaweza kufahamika mpaka sasa, endelea kuwa nami na nitakujuza chochote kitakachojiri juu ya tukio hili.
Habari za hivi punde zinasema kwamba, milipuko ya jana uko eneo la mbagara rangi tatu ilikuwa ni mabomu ya machozi, ambayo ililipuliwa na askali baada ya kushindwa kuwatuliza wananchi waliokuwa na asila kali baada ya kumkamata mwizi nakutaka kumchoma moto mpaka auwawe kwenye eneo la Shimo la mchanga karibu sana na eneo linalojulikana kwa jina la Mbagara kwa mangaya.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI