Featured

    Featured Posts

Loading...

MAMA MWENYE WATOTO WANNE AUWAWA KIKATILI SANA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.


Wiki iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani. Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.


Mwezi wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.


Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni, mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba  na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.

Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10 Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
 Hii ni picha ya muwewe Elia Makumbati ambae mpaka sasa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.Jeshi la polisi mkoani Mara wanafanya juhudi za kila namna kumkamata lakini amekuwa akikimbia mara aonekane Kenya,Botswana na kwengineko lakini bado hajakamatwa.Kwa utakae muona usisite kutoa ripoti zake.Mpaka askari wa upelelezi wa kimataifa interpol ina 

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
          FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top