Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WAKULIMA MBEYA WAPATIWA ELIMU YA UZALISHAJI MBOGA MBOGA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Wakulima na wananchi mkoani Mbeya wameendelea kuneemeka na elimu ya bure ya uzalishaji wa mazao ya mboga, viungo na matunda inayotolewa na Asasi ya wakulima, wafanyabiashara na watoa huduma ya mazao ya horticulture nchini Tanzania (TAHA).
 Aina Mbalimbali za matunda ambazo zimezalishwa na wakulima kutokana na elimu Bora waliyo ipata kutoka TAHA

Wakulima hao wameneemeka na elimu hiyo inayotolewa na maafisa wa ufundi wa kilimo kutoka TAHA kwa ushirikiano na wale wa Barton Tanzania ambao kwa pamoja wameweka kambi katika viwanja hivyo ili kuhakikisha jamii ya wakulima wa mboga kutoka ukanda wa Nyanda za Juu Kusini wanapata elimu ya msingi bora ya uzalishaji wa mboga wenye tija.
Mh. Dr. Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Iringa akipokea taarifa kuhusu mfumo wa taarifa za masoko kutoka TAHA unavyofanya kazi zake kutoka kwa Cyrila Antony Afisa wa Masoko.

"Mpaka sasa tumetembelewa na wananchi na wakulima wasiopungua 460 ambao wamefika katika banda letu hapa Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale wakitaka kujifunza mbinu na misingi ya awali ya uzalishaji wa mazao ya horticulture, hiyo ni ishara njema kwani inaonesha ni kiasi gani wananchi  wanatafuta mbinu fasaha inayoweza kuwakwamua kutoka katika uzalishaji wa mboga wa kawaida mpaka uzalishaji wa tija unaozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa" Alisema Likati Thomas afisa Mawasiliano kutoka TAHA.
Mkuu wa mkoa wa Iringa  Mh. Dr. Christine Ishengoma akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa kilimo wa TAHA Bw Ringo kuhusu uzalishaji wa zao la nyanya 

Akifafanua zaidi kuhusu elimu ya kilimo cha uzalishaji wa mboga kwenye banda la TAHA afisa mawasiliano huyo alisema kuwa wamepanda mazao tofauti katika ploti zilizopo kwenye eneo lao ambapo wakulima na wananchi wanaopata fursa ya kutembelea eneo hilo ujifunza teknolojia mbalimbali za uzalishaji kama vile uzalishaji unaozingatia Mbegu bora zenye tija.
 Watangazaji wa Radio Sweet FM ya Mbeya wakishangaa ubora wa karoti ambayo ni daraja la kwanza inapopelekwa sokoni

Teknolojia nyingine ni pamoja na upandaji mazao unaozingatia nafasi kati ya miche na miche, umwagiliaji kwa njia ya matone(drip irrigation) unaozingatia uhifadhi wa maji na mazingira pamoja na ulimaji wa matuta yaliyoinuka ili kutoa nafasi kwa mizizi ya mimea kupenyeza kwenye udongo ili kujitafutia lishe.
 Teknolojia ya umwagiliaji kwa mfumo wa kilimo cha matone ambao pia unaonesha utengenezaji bora wa matuta, nafasi na usafi

 Vitalu vya mboga na green house kama zinavyoonekana katika picha

Mbali na elimu hiyo ya uzalishaji wa mboga, wananchi wa Mbeya wanaotembelea banda hilo pia wanapata fursa ya kujifunza elimulishe kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia ambaye amekuwa akiwafundisha wananchi juu ya umuhimu wa ulaji wa mboga na faida zake kwa afya ya miili yetu.

Zao la karoti lililopandwa kwenye vitalu vilivyopo ndani ya viwanja vya Nanenane Mbeya kwenye Banda la TAHA

Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 
          FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top