BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
Yanga SC ilitakiwa hadi jana jioni kuwa imethibitisha na kutuma kikosi, lakini haikufanya hivyo na CECAFA ikawasiliana na TFF kuwaambia wapeleke timu nyingine iliyo tayari, ndipo zali likawaangukia Azam FC.
Yanga SC ilitaka kupeleka kikosi cha vijana kwenye nashindano hayo, jambo ambalo CECAFA waliwakatalia wakiwaambia hiyo si michuano ya watoto.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.