Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA WAPEWA SHAVU

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

10520854_764099123654035_8662161622159735181_n
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba za Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake kupitia program maalumu.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori alisema wachezaji wanapaswa kuona fahari kumiliki nyuma au ardhi mjini, si magari.
MPOGOLO PAMOJA NA JACOB
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi huo uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
KATIBU MKUU WA YANGA
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za kisasa zaidi, hivyo ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba, mkitoa kiasi nanyi muwe wamiliki wa nyumba hizo. “Kama utamudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo, NSSF watawapa ufunguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi kwa miaka 15, kisha unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo,” alisema Magori.

MAXIMO, MSAIDIZI WAKE LEIVA, SALVATORY EDWARD
 Aliongeza kuwa hata ikitokea mchezaji akafariki dunia, nyumba hiyo itaendelea kuwa mali ya familia ya mhusika kwani itakuwa imerithiwa huku akisihi wachezaji ambao si wanachama wa NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau. Alisema lengo ni kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa kumiliki nyumba ikiwa ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na manufaa yake wakati anacheza, hata baada ya kustaafu soka.

 Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi. 

          FACEBOOK >>> TWITTER  >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top