ANGALIZO KWA WAFANYA BIASHARA KUPITIA MITANDAO
Huduma ya kufanya miamala ya kibiashara kupitia mtandao inafanya maisha ya leo kua rahisi zaidi kulinganisha na maisha ya awali. Hii ni kutokana na uwezekano wa kufanya miamala hiyo popote pale ilimradi tu uwe unamtandao.
Hili lakua na mtandao kwa Tanzania limeendelea kuwa rahisi hasa baada ya mitandao ya simu kutoa huduma za wavuti inayo sababisha takriban watanzania walio wengi hasa waishio mijini kuweza kupata huduma za mitandao.
Kila teknolojia inachangamoto zake. Na hii ya kufanya miamala kwa msaada wa mtandao pia imekuja na changamoto kadhaa ambazo bado kuna tatizo kubwa la uelewa wa jinsi gani ya kua salama pale miamala ya kibiashara inapofanywa.
Muamala wa kibiashara unapofanyika vibaya unaweza kumgharimu sana mtumiaji kwa kupoteza fedha na hata kupoteza utambulisho wake ( Hii ni pale taarifa zako kupatikana na wahalifu na kutumika vibaya baadae).
Swala la uhalifu mtandao unao athiri miamala ya kibiashara inayofanywa kwa msaada wa mitandao hapo awali ulikua maarufu sana katika nchi za afrika magharibi hasa Nchi kama Nigeria na Ghana – Unaweza kusoma taarifa ya nchi hizo na hali ilivyo hadi sasa kupitia taarifa inayosomeka "HAPA"
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.