Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

GAS KUTEKA SOKO LA MAFUTA HAPA NCHINI TANZANIA.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Nishati na Madini kuanzia mwaka 1972 hadi 1974, Dk Ben Moshi amekiri kwamba ujio wa matumizi ya gesi katika huduma mbalimbali nchini, unaweza kuathiri kampuni nyingi za mafuta zinazofanya biashara nchini.

Hayo aliyasema hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miezi mitatu ya uuzaji wa mafuta ya oil aina ya ‘Castrol’ kwa ajili ya matumizi ya magari yanayotumia mafuta ya dizeli na petroli.

Dk Moshi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi katika kampuni ya mafuta ya PUMA Energy, alisema kampuni za mafuta nchini hazina budi kukubaliana na mabadiliko yanayokuja kupitia mapinduzi ya nishati ya gesiKauli hiyo ameitoa miezi kadhaa tangu taifa liingiwe na mvutano mkali baina ya serikali na wafanyabiashara wa mafuta huku serikali ikituhumu kampuni hizo kutengeneza mazingira ya kuhujumu gesi ili isiweze kupoteza soko la mafuta.

Dk Ben alisema kutokana na changamoto hiyo, mpango mkakati wa muda mrefu ndani ya kampuni hiyo ni kuhakikisha inakuwa tayari kufanya kazi kwa ukaribu na kupokea nishati hiyo ya gesi.“Tuna mpango wa muda mfupi ambao kwa sasa tunahakikisha huduma za PUMA zinasambaa ili kuwafikia wateja wengi, vituo vilivyopo ni 31 tu ambavyo bado ni kidogo,” alisema.

Kwa upande wake, Mshauri wa kitengo cha ufundi katika kampuni hiyo, Gilbert Chacha alisema kwa sasa taifa lina jumla ya kampuni 40 zinazofanya biashara ya mafuta kupitia vituo zaidi ya 1700 vilivyopo sehemu mbalimbali kote nchini.

“Puma ambayo ina hisa ya asilimia 50 za serikali, kwa sasa ina wakala 2000 kote nchini huku ajira zikifikia zaidi ya 700, lengo ni kuhakikisha tunatoa huduma zenye ubora,” alisema Chacha.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top