Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

VIONGOZI MKOA WA PWANI KUSAINI MIKATABA LEO HII

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
MKOA wa Pwani umeingia mkataba na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wenyeviti wa halmashauri juu ya utekelezaji wa mpango wa kupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano. 

Pia mkoa umeingia na viongozi hao kwenye mkataba kwa ajili ya makusanyo ya mapato ambayo waliyapitisha kuwa wana uwezo wa kuyakusanya kwenye halmashauri za wilaya saba za mkoa huo katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2014-2015. 

Wakuu wa wilaya ambao waliingia mikataba hiyo na wilaya zao ni pamoja na Mercy Silla wilaya ya Mkuranga, Fatuma Kimariyo Kisarawe, Nurdin Babu Rufiji, Sauda Mtondoo wilaya ya Mafia, Ahmed Kipozi wilaya ya Bagamoyo na Halima Kihemba wilaya ya Kibaha. 

Akizungumza na watendaji hao kuhusiana na mikata hiyo walioingia na mkoa Mahiza alisema kuwa mikataba hiyo itasaidia uwajibikaji kwa watendaji hao ambao wanawatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo. 

Mahiza alisema kuwa kwa upande wa vifo vya mama wajawazito, watoto wa changa na wale wenye umri chini ya miaka mitano ni tatizo kubwa hivyo mkataba huo utasaidia kupunguza vifo hivyo visivyo vya lazima. 

“Kwa upande wa makusanyo kila halmashauri ilileta makadirio yake ya kukusanya mapato kwenye bajeti ya mwaka 2014- 2015 hivyo ni lazima watimize kusudio lao na hakuna sababu ya kusema wameshindwa kuyafikia malengo hayo ya ukusanyaji wa mapato,” alisema Mahiza. 

Naye mganga mkuu wa mkoa wa Singida ambaye alishinda tuzo ya Rais ya kupunguza vifo vya makundi hayo Dk Doroth Gwajima alisema kuwa vifo vingi vinatokana na uzembe wa baadhi ya watumishi wasio na maadili ya kazi.

Dk Gwajima aliwataka wahudumu wa afya kwenye mkoa huo wa Pwani kumtanguliza Mungu wakati wa utendaji wao wa kazi pia kuzingatia maadili ya kazi zao kwani baadhi ya vifo vinatokana na uzembe na si mapenzi ya Mungu.

Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kuanzia kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mercy Silla na mkuu wa wilaya ya Kisarawe Fatuma Kimario wakisaini mikataba ambayo wameingia na mkoa kuhusu uwajibikaji kwenye sekta za afya na ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zao, 

wakishuhudiwa na wakurugenzi wao ambao wamesimama nyuma yao wakishuhudia tukio hilo juzi. Picha na Johnny Gagarini wa Globu ya Jamii, Pwani.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top