Zungumza na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao, kuwa wa kweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja.
Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati wa kujamiiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu.
Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali wakati wa kujamiiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile mliyoizoea wakati wa kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani).
Kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, ndoa na hata madaktari wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi yao. Tiba ya dawaKutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili
Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk.Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazosababisha madhara kama ya msongo wa mawazo na sonona.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.Kutumia dawa au vilainishi vya ukeni wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza uke kuwa mkavu au kuwasha.
Tiba ya vichocheo (homoni)Dawa za kitaalamu za kuongeza hamu au nguvu atakuandikia daktari baada ya kufahamu kiini cha tatizo. Haishauriwi kutumia bila ushauri wa daktari kwani dawa hizi zina madhara.
