Ndugu msomaji wangu nadhani unafahamu fika yakwamba, Waswahili upenda sana kutumia kauli hii ambayo inasema, "tumia pesa ikuzoee", sasa kwangu mimi napinga kauri iyo kabisa tena kwanguvu zote nikiwa na sababu.
Lengo na sababu za kupinga kauli hiyo nikwamba, kama tunavyojua maisha yamekuwa magimu sana tena kupita kiasi, na ukiangalia sikukuu ndio kwanza zinakaribia, sasa je kama kauri hiyo ikiendelea kutumika je tutapona kweli??
Niwakati wako kama mwana familia kufanya vitu vyenye maana mbele ya jamii inayokuzunguka, nasio kutumia pesa ovyo ovyo pasipokuwa na sababu maalum.
Kiukweli mpaka sasa hapa tulipo hatuna budi kuwa wabunifu, maana bila yakuwa mbunifu utajikuta kilasiku matatizo kwako hayaishi kabisa, kwaiyo basi napenda kutoa angalizo juu ya baadhi ya misemo kwani haina maana kabisa kwa karne tuliyopo ivi sasa.
Napenda kukutakia sikukuu njema yenye amani, utulivu na baraka tele, Mungu azidi kuwa nawe siku zote milele na milele amen.
