Kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha nchi nzima, zimezua kizazaa cha sintofahamu kwa wakazi waishio Mbagala. Chazo ni nvua iliyonyesha jana jioni kuanzia mida ya saa kumi na mbili.
Ambapo huduma ya usafiri wa kutumia barabara ilisimama kwa baadhi ya maeneo, foreni kubwa na kusababisha watumiaji wa usafili huo kutembea kwa miguu kutoka katika maeneo waliyokuwepo mpaka kufika manyumbani kwao.
Juma Khamis ni mmoja wa walio kumbwa na adha ya usafiri siku ya jana, anasema tukio la namna hii si la kushangaza kwa wakazi wa mbagala maana mara nyingi usafiri waga unasumbua sana.
Unavyo tuona hapa tumetoka Kariakoo kwa mguu mpaka hapa, na hakuna mwenye imani ya kupanda gari maana tumebakiza umbali mdogo tufike majumbani kwetu.
Maeneo yaliyo kumbwa na tatizo hili la usafiri nipamoja na Kariakoo to Mbagala, Tazara to Ubungo, Ubungo to Kimala mbezi, Mwenge to Ubungo, ubungo to Kariakoo, posta na maeneo mengine.