Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Bunge la Katiba laanza hii leo.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba leo linaanza wiki ngumu pale litakapohitimisha mjadala wa muundo wa Muungano na kupiga kura kupitisha au kukataa.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba muundo huo wa muungano ndiyo unaotabiriwa kubeba ajenda zote katika mjadala huo wa Katiba. Kwa mara ya kwanza wiki hii Watanzania watashuhudia hatua ya upigaji kura ambayo awali iliibua mvutano mkubwa wakati wa kupitishwa kanuni ili kuamua mfumo gani utumike kati ya kura ya siri na wazi.Katika hili, mjumbe atakuwa na uhuru wa kupiga kura ya wazi au ya siri wakati wa kupitisha sura namba moja na namba sita.

Ili zipite, ni lazima zipate theluthi mbili ya kura kwa kila upande wa Muungano.Hata hivyo, leo Bunge hilo litaanza kwa kumpa nafasi Mjumbe wa Bunge hilo, Tundu Lissu kuendelea kutoa ufafanuzi wa hoja za walio wachache kwenye Kamati Namba Nne.

Ufafanuzi huo wa Lissu uliahirishwa juzi baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kukatika ghafla. Baada ya Lissu kumaliza, kamati zilizobaki ambazo ni Namba Sita inayoongozwa na Steven Wassira, Kamati Namba Saba inayoongozwa na Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi zitawasilisha taarifa zao.

Inatarajiwa kuwa katika kipindi cha mchana, Kamati Namba 10 inayoongozwa na Anna Abdallah itawasilisha taarifa yake na kufuatiwa na ufafanuzi wa wajumbe walio wachache wa kamati hizo.

Kulingana na hali ya mambo ilivyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wataanza kuchangia taarifa za kamati zote 12 katika kipindi cha jioni au kesho asubuhi.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 33 (7), baada ya taarifa ya kamati hizo kuwasilishwa, zitajadiliwa katika kipindi kisichozidi siku tatu. Kama mambo yatakwenda kama ilivyo, inatarajiwa kuwa upigaji wa kura kupitisha sura hizo mbili huenda ukafanyika Ijumaa na hivyo kutegua kitendawili cha muda mrefu kuhusu aina ya muundo wa Muungano katika Katiba Mpya.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright 2025 Mutalemwa Blog | Designed By Code Nirvana
Back To Top