Ni mtu ambaye hata katika familia wanaambiwa, mheshimuni huyu ndiyo mkubwa, msifanyie hivi na vile.
Watoto wa kwanza, hupenda kuonekana viongozi popote wanapokwenda, ni kwa sababu tu ya kujiona kwamba wao katika kuzaliwa na kukua kwao wamekuwa ni watu wa kwanza.
Tangu kuzaliwa mtoto wa kwanza hujikuta ni kiongozi mahali popote na hupenda kuongoza, kupenda kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na kama kilivyopangwa maana ndivyo alikuwa anaagizwa na wazazi kwake kuhakikisha wadogo zake wanatii kile alichoagizwa.
Bila shaka umewahi kusikia mzazi akimwambia mtoto wa kwanza kwamba awaangalie wengine:
Hakikisha wadogo zako wameweka vizuri neti wasije ‘wakaliwa’ na mbu. Hakikisha wamekula na maneno mengi yanayofanana na hayo.
Kwa watoto wa kati, hawa mara nyingi hulelewa ili mradi, hawapewi mapenzi makubwa ukilinganisha na wa kwanza, maana hapo kwa wa kwanza mtu ndiyo kwanza amepata mtoto, amekuwa na furaha kubwa, huwaza kufanya mengi na kadhalika. Kitaalamu watoto wa kati huwa imara zaidi katika kufanya mambo yao, kuliko aina nyingine yoyote ya watoto;
hata hivyo napenda nisisitize kwamba hata kama mtoto atakuwa wa ngapi, wakati mwingine matokeo ya mtoto kuwa na tabia nzuri au mbaya, huchangiwa zaidi na malezi kutoka kwa wazazi wake.
Mtoto wa mwishoAidha mtoto wa mwisho kuzaliwa, kwa asilimia kubwa hujikuta ni mtoto mwenye kulelewa kwa kudekezwa zaidi ya watoto wengine hasa kwa sababu wazazi huwa tayari wamekuwa watu wazima. Ni aina ya watu wanaopenda zaidi raha.
Sherehe hata iwe ndogo, mtoto wa mwisho anapenda kujiandaa hadi unaweza kufikiri ni sherehe ya ajabu.Ninachotaka kueleza hapa ni kwamba ni aina ya watu ambao walio wengi wamedekezwa, wanapenda zaidi raha.
Lakini, wengi ni vigumu kuolewa kwa sababu wanachagua sana. Wanataka sana raha.Kila kitu nyumbani kilikuwa ni kwa ajili yake kwa kuwa yeye ndiye mtoto, hata baada ya kuwa mtu mzima bado anajiona ni mtoto.