ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto-Tanga.
wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepana na basi jingine katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifawa KIA.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio,inasemekana kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni hivi jirani kabisa na kituo cha mafuta kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha.
wakati magari hayo yakijiandaa kuanza safari mara baada ya kuzuiliwa kwa muda ili kupishana na msafara wa Rais Kikwete.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.
Juhudi ya kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha idadi kamili ya waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo.