Tishio la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada ya kundi la kigaidi lililo na makao yake makuu nchini Somalia kuachia video nyingine kwenye mtandao wa Al-Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini Kenya wakati wowote.
kwenye kanda hiyo msemaji wa alshabaab aliye jifunika uso anasema kwamba hawaoni lolote litakalo wa zuia kuingia Kenya hasa baada ya kufanikiwa kutekeleza mauaji katika jengo la west Gate.
mwaka uliopita>>’tumekuwa tukisema tutafika Kenya lakini hivi tayari tushafika si eti westgate ndio tosha bado kuna mamia na mamia ya watu wanaongojewa mahala kama hiyo insha Allah’alisema msemaji huyo.
Huku wakiimbia tutawalipua hadi tuwamalize wanamgambo hao wamesema kwamba wameamua kuungana na wasomali kutetea dini ya Allah,
Wadadisi wa maswala ya kiusalama wanahoji kwamba huenda hawa ni baadhi ya vijana kutoka kwa mataifa ya Afrika mashariki walipewa mafunzo ya itikadi kali na baadaye kupelekwa somalia kujiunga na Alshabaab kutokana na wanavyozungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwenye video hiyo.
Ispekta mkuu wa polisi nchini Kenya bwana David kimaiyo amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha video hiyo na taarifa kamili kutolewa punde tu watakapo pata habari zaidi kuhusiana na video hiyo.