Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ASKOFU AKUMBWA NA UMAUTI.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Askofu wa dayosisi ya Malindi Emmanuel Barbara akiongoza mazishi ya Askofu Boniface Lele katika kanisa la Holy Ghost Cathedral Malindi Aprili 22, 2014.

ASKOFU Mkuu Mstaafu Boniface Lele juzi alasiri alizikwa kwa kuzingatia tamaduni zote za Kanisa Katoliki katika uwanja wa Holy Ghost Cathedral, Mombasa.

Lakini mazishi ya askofu huyo yalikuwa ya aina yake huku kaburi lake likifanana na lile alimozikwa Yesu na watu wengine wa enzi hizo. Pango dogo lilichimbwa kwenye mwamba kutoshea jeneza la marehemu na hakuna hata punje ya mchanga iliyotupwa kaburini humo kama ilivyo kawaida katika mazishi ya kisasa.

Baada ya maombi maalumu kando ya pango hilo dogo, jeneza lilisukumwa ndani kisha pango hilo likafunikwa kwa simiti na vyuma. Kulikuwa na ulinzi mkali kabla ya jeneza la marehemu kuletwa kutoka katika shule ya Loreto ilikofanywa ibada ya wafu.

Umati mkubwa wa watu ulisongamana nje ya kanisa hilo wakitaka kuingia ndani lakini walinzi waliwazuia hadi mwili ulipoletwa.
Polisi wa kawaida, wenzao wa utawala na wengi waliovalia kiraia walionekana juu ya mapaa ya majumba yaliyo karibu na kanisa hilo kama vile Ambalal, TSS Tower na Electricity House huku wengine wengine wakiwa chini.

Mwili ulipofika ulipelekwa moja kwa moja hadi eneo la timbo la mawe yaliyotumiwa kujenga jumba la makasisi na kuwekwa kwenye kivuli kusubiri wakuu wa kanisa kutoka huko Loreto.

Wanahabari walizuiwa kukaribia eneo la timbo kwa hofu kwamba mawe yangeporomoka kutokana na uzito mkubwa juu.
Lakini baadaye ilithibitishwa kuwa mwamba huo ni imara na wanahabari wakaruhusiwa kukaribia. Askofu mwandamizi wa Jimbo la Malindi Kasisi Emmanuel Barbara aliwasili na maaskofu wengine na wakateremka kwenye timbo hilo kuanza sherehe hiyo.

Jeneza lilikuwa limeteremshwa na wanachama wa chama cha wanaume cha kanisa hilo na kuwekwa kando na pango alimopumzishwa Askofu Lele.
Askofu Barbara akisaidiwa na mapadri aliongoza maombi ya mwisho kuombea roho ya marehemu ilale mahali pema peponi. Alinyunyizia maji matakatifu mwili ukiwa ndani ya jeneza na kuufukiza ubani kwa mujibuni wa desturi za Kanisa Katoliki.

“Tukimuaga ndugu yetu Askofu Emeritus Boniface Lele, tunajua ameenda kumuona Baba Mungu uso kwa uso nasi tunatumai kujiunga naye katika ufalme wa milele kwa baba,

” akamaliza Askofu Barbara.VyumaBaada ya sherehe hiyo fupi, maaskofu, mapadri na watawa waliwapisha Wakristo wengine ili watoe heshima zao za mwisho.
Hatimaye jeneza liliwekwa pangoni na waumini wakakafuatana kwa foleni na kupita karibu nalo huku wakitoa heshima za mwisho.Walipomaliza, mafundi waliitwa na wakaanza kufunga kwa vyuma kwenye kiingilio cha pango.

Waziri wa Ardhi, Bi Charity Ngilu ambaye alisoma hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta, alishangaza wengi alipomkumbatia hasimu wake wa kisiasa Kalonzo Musyoka huku umati ukishangilia.

Kulikuwa na vipindi vya ucheshi, hasa pale msemaji wa Dayosisi ya Mombasa aliposema marehemu alipenda kibao cha zilizopendwa kwa jina Rebecca Wanisumbua.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top