Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Mawakala wa radio jamii kutaja faida za mladi wa sida pangani.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya.



Mawakala wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .


Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.

Mmoja wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,” alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.

Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.

Katika kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa na vipindi vya redio.


“Sisi baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone” tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.

Sospeter Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.

Sabina Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kabla ya mafunzo haya kuanza. 


Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki kituo cha Sengerema FM redio.

“Mimi nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo, bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali ya vijijini hususan ya maendeleo”.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top