Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Stephen Baldwin amtumia ujumbe Rihanna.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mwigizaji nyota wa nchini Marekani Stephen Baldwin amemtumia ujumbe maalumu kutoka kwa Roho mtakatifu mwimbaji maarufu wa muziki wa nje ya kanisa Rihanna kutokana na wimbo wake uitwao "What Now" ambao unapatikana katika album yake iitwayo 'Unapologetic' aliyoitoa mwaka juzi.

Kupitia anuani yake ya twitter jumanne hii mwigizaji huyo aliandika kwamba huwa hana kawaida ya kufanya kile ambacho anakifanya(kuandika ujumbe) huo, lakini ameiona video ya wimbo wa 'what now' ya mwimbaji Rihanna ambayo mwishoni kuna mwanga umepita ukionyesha msalaba, huku
Stephen Baldwin.


mwimbaji huyo akimalizia kwakusema
hajui aende wapi" na kwamba Roho mtakatifu anajibu kwamba "ni kweli unajua, umenifahamu mimi kitambo sasa toka ulipokuwa mtoto, unakumbuka jina la Yesu, ni nuru ya uso wako, ni furaha ya moyo wako, rudi kwa Yesu" ndivyo alivyoandika mwigizaji huyo huku chanzo cha habari hii kikisema hapana shaka ujumbe huu ulikuwa mahususi kwa mwanadada huyo ambaye jina lake la kuzaliwa ni Robyn Rihanna Fenty.

Baldwin ameongeza kwamba "pia kama ukipata nafasi ikiwa ni dakika ya 3:29 katika video iliyopo YouTube, najisikia Roho mtakatifu ananiambia kitabu cha Yohana 3:29

Mwigizaji huyo ambaye alimkabidhi Yesu maisha yake baada ya tukio la kigaidi la septemba 11 mwaka 2001 huko nchini Marekani, alitoa ujumbe huu kwa wafuasi wake 35,000 katika anuani yake ya twitter akiwataka kuusoma ujumbe huo huku pia ikiwa haijulikani kama moja ya lengo la mwigizaji huyo ni kukutana na Rihanna kisiri ili kumuhubiria injili ya Yesu.

Rihanna ambaye amekulia katika mazingira ya Kikristo katika visiwa vya Barbados inasemekana hataki kuweka bayana imani yake mbele za watu kwakuogopa kupoteza mashabiki ambao wamejigawa katika makundi mbalimbali yakiwepo ya wasiomwamini Mungu, wanaomwamini na wale wa imani nyingine.

Stephen Baldwin akitoa ushuhuda wake kabla na baada ya kuokoka.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top