Michezo miwili iliyokuwa ikifuatiliwa na wapenzi wa mpira wa miguu nchini ilimalizika kwa watani wa jadi kujikuta wakipoteza michezo yao.
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo chini
Azam 2-1 Simba, Mgambo 2-1 Yanga
Mbeya City 1-0 Prisons.
Katika mchezo uliofanyika uwanja wa Mkwakwani, mabingwa watetezi Young Africans Sports Club wamefungwa na maafande wa Mgambo kwa mabao ya Fully Maganga (dakika 1) na Malima Busungu (Dakika 69, penati) wakati bao la Yanga lilifungwa na nahodha Nadir Haroub katika dakika ya 50 kwa mkwaju wa penati.
Katika mchezo huo Mchezaji wa Mgambo Mohammed Neto alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kukataa kukaguliwa baada ya wachezaji wa Yanga kulalamika kuwa amebeba kitu kilichohisiwa kuwa hirizi.
Uwanja wa Taifa vinara wa ligi Azam wameendelea kujichimbia kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba kupitia mabao ya Khamis Mcha (Dakika ya 16) wakati Simba wakisawazisha kabla ya mapumziko kupitia kwa Joseph Owino wakati John Bocco aliwahakikishia Simba ushindi kwa bao maridadi katika dakika ya 56.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI