Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Haya ndio matunda ya mpango wa Big Results Now.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, leo Machi 28, 2014.

Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.

Serikali imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu.

Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.   

Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia.

Alisema huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha  viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki. 

Aidha, viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana.
Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka.

Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top