Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe ameagiza Polisi nchini kumuachia msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutoa wimbo usio na maadili, Waziri Mwakyembe amesema Rais ameshauri wimbo wa ‘WAPO’ auboreshe kwa kutaja na wakwepa kodi.
BREAKING:Waziri Mwakyembe ameagiza polisi kumuachia Nay wa Mitego, asema Rais ameshauri wimbo wa 'WAPO' auboreshe kwa kutaja na wakwepa kodi.Rais Magufuli abariki ngoma ya Ney ipingwe redioni/TV
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Mwakyembe amesema Rais John Magufuli ameruhusu wimbo wa Ney wa Mitego"WAPO" upigwe vyombo vyote na pia uongezewe vionjo ikiwemo rushwa na mengine.
Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na Wandishi wa Habari mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii. Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies