Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage atofautiana na wamiliki wa malori nchini, habari kamili iko hapa

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage jana alitofautiana na wamiliki wa malori aliposema upungufu wa mizigo ni tatizo la muda duniani, wakati wafanyabiashara hao wamesema ni vigumu kuwarejesha wenye mizigo waliokuwa wakitumia Bandari ya Dar es Salam ambao wamehamia bandari za Mombasa na Beira.

Waziri Mwijage alisema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa), alipowaeleza hali ya kupungua mizigo inaweza kuchukua mwaka na zaidi na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.

Waziri Mwijage aliwataka wamiliki hao wa vyombo vya usafirishaji kusitisha huduma hiyo kwa sasa hadi hali itakapotengemaa.

“Ushauri wangu kwenu ni kusimamisha malori yenu na kuyatunza vizuri kwa sababu mizigo haipo hivi sasa, hali ikirejea muendelee kufanya biashara,”alisema. Alisema kukosekana kwa mizigo ni anguko dogo la uchumi wa dunia ambalo baadaye litaimarika.

“Niwasihi msiangalie sana muda, inaweza kuchukua mwaka mmoja au zaidi kidogo ya hapo ili kurudia hali ya zamani, lakini msikate tamaa,” alisema Mwijage.

Waziri Mwijage alisema kushuka kwa bei ya madini kwenye soko la dunia kumesababisha nchi kama Zambia na Congo DRC kupunguza mizigo inayopitia kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

 Alisema baadhi ya migodi ya nchi hizo imesitisha uzalishaji na kusababisha mizigo ya kusafirisha ipungue kwa kiasi kikubwa. Waziri pia alisema mazao ya biashara yameshuka bei kwenye soko la dunia na hivyo kupunguza uzalishaji na kuleta athari katika sekta ya usafirishaji.

Lakini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NMC Tracking, Natal Charles alisema itachukua muda mrefu kuwarejesha watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu waliondoka kwasababu ya ushindani wa kibiashara uliopo kwenye bandari nyingine.

“Kukosekana kwa mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam ni changamoto kwetu wenye malori kwa sababu wapo waliokopa benki ili kuyanunua magari hayo na sasa wako katika hatari ya kufilisika,” alisema.

Alisema pia wako baadhi ya wamiliki wa malori ambao wameshafilisika kutokana na kukosa mizigo.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vya nje, moja ya sababu inayohusishwa na kuathirika kwa usafirishaji wa mizigo duniani ni kufilisika kwa kampuni kubwa ya meli ya Korea Kusini inayoitwa Hanjin, ambayo inashika nafasi ya saba katika biashara hiyo duniani.


Kufilisika kwa kampuni hiyo kumesababisha meli za kampuni hiyo kunyimwa kibali cha kushusha au kupakia mizigo kutokana na kutokuwa na uhakika wa kufikishwa inakoelekea, limeandika gazeti la The Guardian la Uingereza.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mwijage aliwashauri wamiliki wa malori kuangalia aina nyingine ya uwekezaji, kama kujenga viwanda.

“Wekezeni katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kulingana na uwezo na fursa ya kila mmoja wenu,” alisema.

Alisema anawafahamu baadhi ya wanachama wa Tatoa ambao wameanzisha viwanda vya maziwa, maji, kutengeneza mabomba na kusaga mahindi ili kupata unga.

“Mwekezaji makini hawezi kung’ang’ania biashara ya aina moja kwani inapoleta hasara anaachana nayo na kuendelea na ile inayomletea faida,” alisema.

Hata hivyo, Mwijage aliwataka Tatoa kupeleka mapendekezo yao serikalini ya namna ya kuboresha sekta ya usafirishaji huku wakitoa mifano halisi ya namna ya kuiboresha sekta hiyo.

 “Wizara yangu ndiyo yenye dhamana ya kuboresha wepesi wa kufanya biashara. “Nileteeni masuala yote yanayowakwamisha nami nitayawasilisha kwenye mamlaka husika,” alisema waziri huyo.

Alisema kama malori ya mizigo hayasafiri, biashara ya vipuri itashuka na matumizi ya mafuta yatashuka na hivyo kuziathiri sekta nyingi.

Alisema malori yamekuwa yakisaidia kuongeza mapato ya Serikali na kutunisha mfuko wa barabara.

 Awali, Mwenyekiti wa Tatoa, Elias Lukumay alisema wamiliki wa malori wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maeneo ya kuegesha malori wakati yakisubiri kupakia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema mara kwa mara wanapoegesha kwenye maeneo ya barabara jirani na bandari hiyo wamekuwa wakikamatwa na kutozwa faini.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top