Tazama Matukio mbalimbali yaliyofanyika kweye mashindano ya SUMATRA CCC day katika viwanja vya Benjamin Mkapa High School tarehe 29/10/2016.
Lengo la mashindano haya ni kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na jamii nzima jinsi ya kujiepusha na ajali kwenye vyombo vya usafiri na kauli mbiu ya mwaka huu kwa mkoa wa dar es salaam inasema hivi, "hatutaki ajali ni haki na wajibu wetu sote kujilinda"
Mashindano haya yaliambatana na zoezi la kujitolea damu kwa Wanafunzi chini ya usimamizi kutoka kitengo cha damu salama.
Nicholous kinyariri, afisa elimu wa sumatra CCC.
Shule zilizoshindanishwa katika mashindano haya ni sita tu kama zinavyoonekana hapo chini
1. Benjamin Mkapa high school
2. Kibasila sekondary school
3. Makongo sekondary school
4. Mibulani shule ya msingi
5. Oyster bay shule ya msingi
6. Msimbaz boys shule ya msngi.
Huyo mwanafunzi kwenye picha anaitwa Deborah hugo ni Mwanafunzi wa Benjamin mkapa high school.
Michezo iliyoshindanishwa kwenye shule izi ni maigizo, nyimbo pamoja na ngonjera.
Martha Sepeku,ni mwalimu mlez wa sumatra club shule ya msingi Msimbazi boys na pia Mwenyekiti wa walimu walezi wa vilabu vya sumatra CCC mkoa wa Dar es salaam.
Na kati ya shule izi sita washindi ni kama wafuatao hapo chini.
1. Msimbazi Boys primary school
2. Makongo secondary school
3. Benjamin Mkapa high school.