Featured

    Featured Posts

Loading...

UZURI NA UMBO LAKO SIYO FIMBO YA KUMPIGA MUME WAKO, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Siku zote nimeweka mdomon neno linalosema kuwa mwanaume ni.kifaa adimu kwa sababu watu wanamaliza waganga,wanafanya matambiko ili wapate waume. Cha ajabu kuna wanawake ambao Mwenyenzi Mungu
amewapa wanaume lakini hawajitumi wapo wapo tu!

Mfano, Unakuta mume anafua mwenyewe,mume njaa inamuuma mke yupo anaangalia TV au kaenda kuzurura Mume amevaa nguo chafu kisa mke hajali suala la kufua. Jamani mume kwa mke ni kama mtoto anatakiwa ale kwa wakati,avae nguo safi.

Kuna baadhi ya wanawake wanadhani uzuri walionao na sifa zote walizojaaliwa kuwa nazo ni fimbo ya kumpigia mume.

Kumbuka kuwa kuna wanawake wazuri sana kiasi kwamba ukiwaangalia wewe mwenyewe unawakubali lakini wanajituma ipasavyo kwa waume zao. Sasa wewe ni nani mpaka ubweteke hivyo?.

Hebu jitaidi kumjali mumeo, isipite siku hujamjulia hali, kama yupo mbali na wewe mtumie hata ujumbe wa kumwambia kuwa umemkumbuka Muulize amekula nini,mkumbushe kuwa muda wa kula umefika na sms nyingine za kuonesha kuwa umemkumbuka.

Utakuta mwanamke kutwa nzima anazurura,mara yuko Kariakoo anatafuta madera,mara kaenda kwa shosti wake
magomeni, akirudi nyumbani kachoka.

Mume sasa anataka huduma unashangaa mke anadai kachoka,akifuatilia kachoshwa na kipi,eti sababu ya kuzurura kutwa nzima,huko ni kujiaibisha.

Mke kama ni mama wa nyumbani au umewahi kurudi kazini au uko 'off' tulia nyumbani ukimsubiri mumeo. Fanya usafi wa hapa na pale,kiandae chumba chako kwa kutandika kitanda,pulizia manukato,udi mzuri,asmini nk, mambo nga'ari ng'ari.

Mumeo akirudi akukute umeshajiandaa kimawazo kumpokea. Siyo anarudi anakuta nyumba iko vululuvululu,wewe
mwenyewe unanuka jasho,utaachika kama siyo kutafutiwa mke mwenza shoga.

Lakini pia sio mbaya ukatenga muda wa kumkata kucha mumeo,kumsafisha masikio kwani mbali na kwamba kufanya hivyo ni kumfanya awe safi,pia ni mapenzi kunaamsha hisia.

Mwisho nakukumbusha mwanamke mwenzangu kwamba fanya yote lakini tendo la ndoa ni haki ya mumeo na ni mhimili wa ndoa.

Kilichokufanya ukaaicha familia yako na kwenda kwa mumeo siyo kula wala kufuata mali,umefuata haki hii Kwa maana hiyo basi,isitokee hata siku moja ukamwambia mumeo 'NINECHOKA' wakati yeye anahitaji.

Hii kusema mara unaumwa,mara umechoka mara hujisikii ni kosa kubwa na wengi wamejikuta wakitafutiwa michepuko kwa kutokuwa makini katika kuwatimizia waume zao.

Kumbuka kwamba licha ya uzuri wako na kujaaliwa kuwa na umbo zuri usilete maringo kwa mumeo. Uzuri wako hauwezi kuishika ndoa, wajibika kama mke ili umfanye mumeo aamini amepata mke kwa maana halisi ya mke na siyo toi,upo hapo shoga, ukisema wanin wako wanasema watampata lini.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top