Naye mwanasheria wa CHADEMA akizungumzia barua walizopewa amedai barua hizo zina muhuri wa siri hivyo kuzionyesha hadharani inaweza kuwa ni kosa kwa kuwa kuna sheria ya usalama wa taifa inayokataza kuonyesha hadharani barua zenye muhuri wa siri
Lakini pia amesema inaweza isiwe ni kosa kwa kuwa tume ya Nyalali ilishapendekeza sheria hiyo irekebishwe kwa kuwa inakiuka uhuru wa kupeana habari na hivyo ipo kinyume na katibalakini haijafanywa hivyo mpaka sasa hivi, lakini wao wanafanya kwa kuwa katiba inawapa uhuru wa kusambaza habari na watazigawa barua hizo kwa waandishi wa habari
Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu tamko la Magufuli la kuataka asijaribiwe lakini wao wana mpango wa kufanya maandamano amesema hakuna mtu anayetaka kumjaribu Magufuli wala kukamatwa na kupelekwa mahabusu bali wanafanya kile ambacho katiba inawaruhusu kufanya na kupinga jambo linalofanywa na rais kama wameona halipo sawa, kama kufanya hivyo Magufuli anafikiri wanamjaribu hiyo ni sababu zake
Amesema kuwa wanaomshauri rais waanze kumsomesha sheria kabla hajatoa kauli yoyote hadharani kwa kuwa ni aibu na rais anajifedhehesahana anawafedehesha wao anaowaongoza na kuhoji ni nani anayemjaribu?
ameendelea kusema wamefanya mikutano ya kisiasa tangia zama za Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hawakukatazwa na kushangaa Magufuli anawambia wasimjaribu. Ametaka wanaomshauri wapate mishahara yao kihalali kwa kuwa kauli za rais zinatia aibu wananchi na zinamtia aibu yeye
Katibu mkuu aendelea kuzungumza
Katibu mkuu amesema wamepata wito wa kwenda kwenye ofisi ya tume ya haki za binadamu na watahudhuria kikao hicho ambacho kikao hicho kina ajenda ya kujadiliana mustakabali wa haki ya mikutano ya hadhara na maandamano na kusikiliza kuhusu UKUTA
Katibu mkuu wa CHADEMA akizungumzia kauli ya Magufuli ya kuzuia UKUTA amesema kazi ya chama cha siasa ni kukaa na kuangalia serikali inaelekea kwenye uelekeo shaihi kama inaelekea kwenye uelekeo sahihi wataipongeza lakini kama haielekei wataipigia kelele hadi ijirekebishe.
Amesema kama mkuu wa nchi kama ameona sheria ya vyama vya siasa inamchelewesha asilete maendeleo basi aibadili. Ameendelea kusema raia yoyote ambaye ni mzalendo chochote atakachofaya kwanza ni kutii sheria za nchi na hakuna aliyepo juu ya sheria, hata rais ni rais kwa kuwa katiba ndio imempa mamlaka hayo
Amedai suala la UKUTA sio la CHADEMA peke yake ni la kila mwananchi na kwa kuwa kuna ambao wamesimamishwa kazi bila kufuata utaratibu, kuna ambao mali zao zimekamatwa bila kufuata utaratibu na wengine wameambiwa walazwe bila kufuata utaratibu
Amesema kuna viongozi wa CHADEMA wanaendelea kukamatwa kwa kujenga ukuta akisema katibu wa kanda ya ziwa amekamatwa na kufikishwa mahakamni na viongozi wengine pia wamekamatwa katika harakati za kujenga ukuta lakini wataendelea hadi hapo itakapoonekana ni nani anatekeleza sheria na ni nani anayevunja
Tundu Lissu ameendelea kusema watajibu barua hiyo na wataisambaza kwa waandishi majibu ya barua hiyo ila wataonyesha mshangao wao kwa barua hiyo ilivyoandikwa bila kuzingatia taaluma na mtu aliyekuwa jaji wa mahakama kuu na inawezekana kuna watu wengi wameumizwa na maamuzi yake aliyokuwa anayatoa kama jaji kutokana na upungufu wa weledi
Akizungumzia kuhusu madai ya TCRA kutaka kuzuia mawasiliano yake kwenye mitandao ya kijamii amesema ni kweli amesoma taarifa hizo na kudai mamlaka hiyo haina kazi ya kuminya uhuru wa tu kuwasiliana bali kudhibiti na kudai wanataka kumfungia kwa kosa la kusema kuwa amekamatwa baada ya kutoka kufanya mkutano kwenye jimbo lake na polisi hawakufurahi kusambaa kwa taarifa hizo amesema hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzuia mawasiliano yake kwenye mitandao ya kijamii
Amesema kama TCRA wakifuata mkumbo wa kutokufuata sheria kama mkuu wa nchi anavyofanya ili kumfurahisha atakabiliana nao.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies